Friday, May 26, 2017

2017 FA Cup FAINALI
Uwanja: Wembley Stadium, London
Tarehe: Jumamosi Mei 27
Saa: 1930 Bongo Taimu
Arsenal v Chelsea
++++++++++
FACUP-FAINALI2017JUMAMOSI Wembley Stadium Jijini London, ipo patashika ya mwisho kabisa ya Msimu huu wa Soka huko England kwa kuchezwa Fainali ya FA CUP ambayo ni Fainali ya 136 tangu Mashindano haya yaanzishwe Mwaka 1872 na ndiyo Mashindano makongwe kabisa Duniani.
Safari hii Fainali hii ya FA CUP, sasa ikibatizwa EMIRATES FA CUP kwa sababu za kiudhamini, itawakutanisha Mabingwa Wapya wa England Chelsea na Arsenal ambao walimaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Arsenal walifuzu kutinga Fainali hii walipoifunga Man City 2-1 katika Dakika 120 za Mchezo baada ya Sare ya 1-1 katika Dakika 90 na Chelsea kuinyuka Tottenham Hotspur 4-2 katika Nusi Fainali nyingine, Mechi zote zikichezwa Wembley.
Wakati Chelsea wakitinga Fainali hii huku wakiwa na morali kubwa ya Ubingwa, Arsenal wao wanaomba tu wamalize Msimu wao wa balaa na taabu kwa kubeba Kombe hili kwa mara ya 13 na hivyo kuipiku Manchester United na kuweka Rekodi ya kulitwaa mara nyingi kupita Klabu yeyote.
Arsenal na Man United ndizo sasa zinazoshikilia Rekodi kwa kubeba FA CUP mara 12 kila mmoja.
Msimu huu kwa Arsenal umekuwa mgumu mno kwao hasa baada ya Meneja wao wa muda mrefu, Arsene Wenger, kusakamwa akitakiwa ang’oke na baadhi ya Mashabiki huku pia Timu yenyewe ikikosa Msimu ujao kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya kwanza katika Miaka 20.
Kwa Chelsea mambo ni murua na sasa wanalenga kutwaa Dabo kwa mara ya kwanza tangu 2010 walipobeba Ubingwa wa Ligi na FA CUP na kutia Kabatini Kombe kubwa la 15 tangu Mmiliki wao Roman Abramovich alipoinunua Chelsea Mwaka 2003.
++++++++++
JE WAJUA?
-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
KUANZIA MSIMU HUU – KUANZIA Robo Fainali:
-Hamna Marudiano ikiwa Timu zipo Sare baada ya Dakika 90. Sare itafuatia Dakika za Nyongeza 30 na kama Gemu bado Sare, zitafuatia Penati ili kupata Mshindi.
-Kila Timu inaruhusiwa kubadili Wachezaji si zaidi ya Wanne lakini huyo wa Nne ni pale tu Gemu ipo Dakika za Nyongeza 30.
++++++++++
FACUP-SAFARI
Hali za Timu
Wakati Chelsea mambo ni shwari, Arsenal wana hali ngumu hasa kwenye Difensi yao kwa kuwakosa Laurent Koscielny, Gabriel na ipo hatihati kuhusu kupona kwa wakati kwa Majeruhi Shkodran Mustafi.
Koscielny yeye yupo Kifungoni Mechi 3 baada ya Jumapili iliyopita kupewa Kadi Nyekundu walipocheza na Everton kwenye Mechi yao ya mwisho kabisa ya Msimu wa Ligi wakati Gabriel akiumia katika Mechi hiyo hiyo.
Kuumia huko kwa Gabriel katika Mechi hiyo kulitoa mwanya kwa Mjerumani Per Mertesacker kucheza Mechi yake ya kwanza ya Msimu baada kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza Goti lake.
Nini Mameneja Wanasema
-BOSI wa Arsenal Arsene Wenger: "Haitakuwa Mechi yangu ya mwisho kwani lolote litakalotokea nitabaki kwenye Soka. Je itakuwa ni kuagwa vizuri tukishinda? Hapana, Siku zote nataka nishinde Gemu ifuatayo. Napenda ushindi na napenda Klabu yangu ifanye vyema. Nataka tutwae Kombe kwa Klabu yangu. Hili si langu ni Klabu!”
-BOSI wa Chelsea Antonio Conte: "Kutwaa Ubingwa Msimu huu ni kitu kikubwa. Msimu huu utakuwa mkubwa zaidi tukitwaa FA CUP. Hii ni nafasi bora kushinda na kutwaa Dabo! Lakini ukiniuliza nani ana nafasi nzuri kubeba Kombe ntakwambia ni Arsenal!”
TAKWIMU MARIDHAWA:
-Hii ni Fainali ya Pili ya FA CUP kuzikutanisha Arsenal na Chelsea. Mwaka 2002 Arsenal iliichapa Chelsea 2-0 huko Cardiff kwa Bao za Ray Parlour na Freddie Ljungberg.
-Ushindi kwa Arsenal, utawafanya Arsenal wawe wamebeba FA CUP mara 13 na kuipiku Man United, iliyotwaa mara 12, na wao kuweka Rekodi ya kulichukua mara nyingi Kombe hili.
-Ikiwa Chelsea watashinda, hii itakuwa ni mara yao ya 8 kubeba FA CUP na kufungana na Tottenham wakishika Nafasi ya 2 kwa wingi.
-Ikiwa Arsenal watashinda Fainali hii, itakuwa ni mara ya 3 kwa Arsene Wenger kubeba FA CUP katika Misimu Minne na kuweka Rekodi ya kulibeba mara nyingi.
Kwa sasa Wenger anafungana na George Ramsay wote wakishinda mara 6.
-Antonio Conte atakuwa Meneja wa 5 toka Italy kubeba FA CUP na Watatu kati ya Wanne kufanya hivyo walikuwa na Chelsea. Hao ni Vialli, Mwaka 2000, Ancelotti 2010, Mancini 2011 na Di Matteo 2012.
-Chelsea hawajapoteza Fainali yao yeyote ya FA CUP katika 4 zilizopita zilizochezwa Wembley (Walishinda 2007, 2009, 2010 na 2012). Mara ya mwisho kufungwa Fainali ya FA CUP ni 2002 na tena ilikuwa ni mikononi m

0 comments:

Post a Comment