Friday, May 26, 2017

MAN CITY YAWAACHA GAEL CLICHY, BACARY SAGNA, JESUS NAVAS NA WILLY CABALLERO!

CITY-PEP-6Gael Clichy, Bacary Sagna, Jesus Navas na Willy Caballero wanaondoka Manchester City baada ya Mikataba yao kumalizika.
Wachezaji hao hawakupewa Mikataba Mipya.
Clichy, Fulbeki wa Kushoto, ameichezea City zaidi ya Mechi 200 tangu ajiunge nao Mwaka 2011 akitokea Arsenal na Mwaka 2012 alikuwemo Kikosini walipotwaa Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza baada Miaka 44.
Fulbeki wa Kulia, Bacary Sagna, alijiunga na City Mwaka 2014 akitokea Arsenal na kuichezea Mechi 85.
Winga Navas, aliejiunga kutoka Sevilla Mwaka2013, alitwaa Ubingwa wa England akiwa na City Mwaka 2014 na kuanza Mechi 117.
Kipa Caballero amechuza Mechi 48 na kati ya hizo 27 chini ya Meneja Pep Guardiolla Msimu huu.
City haijatangaza akina nani Wapya watakuja kuziba mapengo hayo ingawa sasa inaonyesha Wamiliki Matajiri wa City wanataka Guardiolla asuke upya Kikosi chao

0 comments:

Post a Comment