- 26 Mei 2017

Mabingwa wa taji la Europa ligi
msimu huu klabu ya Manchester United inatarajiwa kuweka kikomo cha
kufanya usajili kwa wachezaji watatu au wanne muhimu katika dirisha
kubwa la usajili
Meneja wa United Jose Mourinho amesema makamu
mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward anajua wachezaji wanaotakiwa kwa
zaidi ya miezi miwili iliyopita."Ed Woodward anayolisti yangu ya wachezaji ninaowataka ," alisema meneja huyo baada ya mchezo wa Europa ligi dhidi ya Ajax .
Mourinho anataka kuongeza changamoto katika safu ya ulinzi na ushambuliaji ili kuweza kuwania taji la ligi kuu ya England msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment