Wednesday, June 28, 2017




Details by alanus
Created: Wednesday, 28 June 2017 08:05
>JUMATANO NI GERMANY v MEXICO!


LEO huko Russia ipo Nusu Fainali ya Kwanza ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara itakayochezwa Uwanja wa Kazan Arena, Mjini Kazan kati ya Mabingwa wa Ulaya Portugal na Mabingwa wa Marekani ya Kusini Chile.
Portugal wataingia kwenye Mechi hii wakimkosa Beki wao Pepe ambae amefungiwa Mechi 1 baada ya kuzoa Kadi za Njano 2.
Lakini tegemeo kubwa la Portugal ni Mashambulizi yao wakiongozwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo ambae amepiga Bao 2 kwenye Mashindano haya na kusaidia 1 na ndie anaeongoza katika Ufungaji.
Portugal na Chile zimekutana mara 3 na Portugal kushinda 2 na Sare 1.
Lakini Chile ya sasa, ambao wamekuwa Mabingwa wa Marekani ya Kusini mara 2 mfululizo, ipo kwa Wachezaji wao mahiri kina Arturo Vidal; Eduardo Vargas na Alexis Sanchez.
Nusu Fainali ya Pili ya Mashindano haya itachezwa Alhamisi kati ya Germany na Mexico.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Portugal: Rui Patricio; Raphael Guerreiro, Bruno Alves, Jose Fonte, Cedric; Andre Gomes, William Carvalho, Adrien Silva, Gelson Martins, Cristiano Ronaldo, Nani
Chile: Claudio Bravo; Mauricio Isla, Gary Medel, Gonzalo Jara, Jean Beausejour; Pablo Hernandez, Marcelo Diaz, Charles Aranguiz, Arturo Vidal; Eduardo Vargas, Alexis Sanchez
REFA: Alireza Faghani [Iran]
++++++++++++++++
FIFA KOMBE LA MABARA
Ratiba/Matokeo:
Hatua ya Kwanza
Jumamosi Juni 17
KUNDI A
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Russia 2 New Zealand 0
Jumapili Juni 18
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
Portugal 2 Mexico 2
KUNDI B
Spartak Stadium, Moscow
Cameroon 0 Chile 2
Jumatatu Juni 19
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
Australia 2 Germany 3
Jumatano Juni 21
KUNDI A
Spartak Stadium, Moscow
Russia 0 Portugal 1
Fisht Stadium, Sochi
Mexico 2 New Zealand 1
Alhamisi Juni 22
KUNDI B
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Cameroon 1 Australia 1
Kazan Arena, Kazan
Germany 1 Chile 1
Jumamosi Juni 24
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
Mexico 2 Russia 1
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
New Zealand 0 Portugal 4
Jumapili Juni 25
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
Germany 3 Cameroon 1
Spartak Stadium, Moscow
Chile 1 Australia 1
Hatua ya Pili
Nusu Fainali
Jumatano Juni 28
Kazan Arena, Kazan
2100 Portugal v Chile [NF1]
Alhamisi Juni 29
Fisht Stadium, Sochi
2100 Germany v Mexico [NF2]
Mshindi wa 3
Jumapili Julai 2
Spartak Stadium, Moscow
1500 Atakaefungwa NF1 v Atakaefungwa NF2
FAINALI
Jumapili Julai 2
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
2100 Mshindi NF1 v Mshindi NF2

0 comments:

Post a Comment