Kufuatia
kuondoshwa kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye hivi
sasa yuko kwao Congo, inaelezwa kuwa mabosi wa timu hiyo wanataka kumpa
timu Charles Boniface Mkwasa.
Taarifa
hizo zimekuja ikiwa ligi bado ipo raundi ya kwanza ya msimu katika
ligi, ikitajwa kuwa mabosi hao hawana mpango wa kusajili Kocha mpya
kutoka nje ya nchi kwa kipindi hiki.
Maamuzi
hayo yankuja Yanga wakiwa na nia ya kuwajenga vizuri wachezaji wake
kisaikolojia na kutovuruga zaidi mwenendo wa timu hivyo badala yake
wanataka kuendelea na Mkwasa kwa msimu huu.
Mkwasa
alichukua nafasi hiyo na ameingoza Yanga kucheza mechi moja ya ligi
huku akishinda kwa bao 1-0 ikiwa ni dhidi ya Ndada huko Mtwara.
Kuna
uwekezekano Yanga ikaanza kusaka Kocha mwingine mara baada ya msimu
kumalizika ambaye anaweza akatokea nchi za Afrika Magharibi ama nje
kabisa ya bara la Afrika.

0 comments:
Post a Comment