Thursday, September 13, 2018


Wakati Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakiwa na wastani wa kiwango cha 94 kwenye viwango vya michezo ya video maarufu kama FIFA, Ronaldo amewekwa namba 1 licha ya kulingana na Messi.

Cristiano Ronaldo amekaa namba moja mbele ya Lionel Messi, baada ya kampuni ya EA Sports kutoa makadirio yao ya mwisho ya viwango kwenye toleo la FIFA la msimu wa 2019.

Kwanini Ronaldo amekaa juu ya Messi?
Ronaldo na Messi kwa pamoja wamepata 94 kati ya 100, suala la kasi (Ronaldo 90 vs Messi 88), Mashuti ( Ronaldo 93 vs Messi 91), na nguvu (Ronaldo 79 vs Messi 61) hivyo ndivyo vitu ambavyo vimenfaya Ronaldo kukaa juu ya Messi.


Je nani atatumika kwenye kava la FIFA?
Mreno huyo ambaye mpaka sasa hajafanikiwa kupata bap lolote ndanj ya klabu yake mpya ya Juventus ndiye atakayetumika kwenye kava za FIFA la mwaka 2019.


Je mchezaji ghali zaidi duniani nae vipi?
Nyota wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Brazil Neymar anashikilia nafasi ya tatu kutokana na uwezo wake na ubunifu mkubwa na maudambwi aliyo nayo. Nyota huyo nae ni mmoja wa wachezaji wenye nyota 5.



Klabu gani imepitisha wachezaji wengi top 10?
Real Madrid imeweza kupitisha wachezaji watatu wenye wastani mkubwa kwenye orodha ya nyota bora kumi duniani. Luka Modric, Sergio Ramos na Toni Kroos wameingia kwenye orodha hiyo.

Kutoka Barcelona Messi amesindikizwa na Luis Suarez pekee mwenye wastani wa 91.


Vipi nako ligi kuu ya Uingereza?
Mlinda lango wa Manchester United David de Gea ndiye wa kwanza duniani katika makadirio hayo akiwa na alama 91.

Eden Hazard wa Chelsea na kiungo machachari wa Manchester City Kevin de Bruyne ambaye anashikilia nafasi ya 4 kwa ubora duniani huku Hazard akishikilia nafasi ya 6.

Je Bara la Afrika nalo?
Hakuna mchezaji mweusi kutoka bara la Afrika aliyeingia 50 bora ya FIFA 19. Mohamed Salah ndiye mchezaji pekee kutoka bara ka Afrika aliyeingia katika orodha hiyo akiwa na wastani wa 88. Mchezaji pekee mweusi aliyeingia katika orodha ya wachezaji 100 bora ni Sadio Mane akiwa na wastani 86 akishikilia nafasi ya 60,

Riyadh Mahrez ndiye mchezaji mwingine wa Afrika aliyefanikiwa kuingia 100 bora ya FIFA 19, akiwa na wastani wa 85 akishikilia nafasi ya 99.


Michezo hiyo itatolewa rasmi September 28.

0 comments:

Post a Comment