
Nyota wa tenisi kutoka Urusi Maria
Sharapova, amenyimwa kadi maalumu ya kuingia kwenye mashindano ya French
Open yatakayoanza baadae mwezi huu.
Mkuu wa chama cha tenisi
nchini Ufaransa Giudicelli Ferrandini mwaliko huo ungeliweza kutolewa
kwa mchezaji ambaye ametoka kuwa majeruhi lakini sio kwa aliyefungiwa
kwa kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli.Sharapova, mshindi mara tano wa Grand Slam, alimaliza kifungo cha miezi 15 hivi karibuni na hakuwa na alama za kutosha za kuingia katika droo kubwa ya kushiriki michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment