
Mchezaji namba nne kwa ubora duniani
katika tenisi kwa kina dada Simona Halep amesema ana uhakika wa
asilimia 50 iwapo atakuwa tiyari kushiriki michuano ya French Open
inayoanza wiki ijayo.
Halep raia wa Romania aliumia kifundo cha mguu wakati wa michuano ya Italian Open.''Ninaba Mungu anisaidie sana katika hili,madaktari wanasema nina asilimia 50 za kucheza lakini ninaendelea vizuri tokea Jumapili'' alisema Halep.
Muingereza namba nne kwa ubora Tara Moore hatokuwepo katika michuano hiyo baada ya kupoteza katika hatua ya kufuzu kwa seti 6-2 7-5 dhidi ya Kai-Chen Chang wa Taiwan.
0 comments:
Post a Comment