13june 2017
by alanus
Shirikisho la kandanda duniani
(FIFA) limekataa ombi la klabu ya soka ya Etoile Filante de Garoua
kutoka nchini Cameroon , kuizua timu ya taifa kushiriki katika michuano
ya mabara itakayofanyika tarehe 17 mwezi huu nchini Urusi.Klabu
ya Etoile Filante inayompinga rais wa Shirikisho la soka nchini humo
Tombi Roko Sidiki, imesema kiongozi huyo hana mamlaka dhidi ya timu
hiyo.
FIFA imesema inafahamu kuwa kuna changamoto ya uongozi
katika Shirikisho hilo la nchini Cameroon (FECAFOOT) lakini inaendelea
kumtambua Sidiki kama kiongozi halali wa Shirikisho hilo.
0 comments:
Post a Comment