Rushwa ilionekana kutawala wakati wa mchakato wa kutafuta taifa litakaloandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022, ambapo kesi hiyo ilionekana kama inapoa poa lakini sasa mapya yameibuka kuhusu madududu yaliyotawala mchakato huo.
Jarida maarufu la nchini Ujerumani liitwalo Blid limetoa taarifa nyingine zinazoonesha mchakato huo jinsi ulivyotawaliwa na rushwa kwani hadi mtoto wa miaka 10 alitumika kuhifadhi pesa chafu kwa ajili ya kufanikisha mchakato huo.
Inasemekana siku chache kabla ya mchakato huo kuanza, kiasi cha pesa cha zaidi ya dollar milion 1.8 kiliingizwa kwenye saving account ya mtoto wa afisa mmoja wa juu wa FIFA pesa ambazo hazijajulikana chanzo chake lakini Blid wamezihusisha na mchkato huo.
Blid pia linasema linayo taarifa ambayo hapo mwanzo iliondolewa ya Michael Garcia ambae alikuwa wakili wa wa Fifa aliyekuwa akihusika na masuala ya uchunguzi ya maadili katika taasisi hiyo lakini 2014 Garcia alibwaga manyanga.
Inasemekana Garcia alibwaga manyanga kutokana na kutofurahishwa na matokeo ya ripoti yake ambapo anaamini katika hukumu iliyotolewa na hakimu Hans Joachim Eckert ilipunguza mambo mengi sana haswa kutoka ukurasa wa 430.
Katika ripoti hiyo ukurasa wa 42 uliiondolea Quatar tuhuma za rushwa lakini gazeti la Blid linasema lina taarifa kamili kuhusu mchakato huo huku pia likianika safari za maafisa wa FIFA kusafirishwa hadi Brazil katika jiji la Rio Di Jeneiro.
Ripoti zinasema maofisa hao wa FIFA walisafirishwa na ndege binafsi ya shirika moja kutoka Quatar kwenda tu Brazil na ikumbukwe Quatar waliowapa ndege maofisa hao nao pia walikuwa moja ya mataifa yaliyokuwa yakitafuta nafasi ya kuandaa mashindano hayo.
Blid halijaweka wazi wazi kwamba Quatar na Russia walihusika moja kwa moja na rushwa lakini wanasema ripoti hiyo ya Garcia katika ukurasa huo wa 430 ulikuwa una msingi wa kukamata viongozi wa juu wa FIFA lakini hilo halikutendeka ipasasavy
0 comments:
Post a Comment