7june2017

Kiungo wa Simba Mwinyi Kazi Moto
(kulia) akiwania mpira na Amani Kyata, wa Nakuru All Stars, wakati wa
mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja
wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Beki wa Nakuru All Stars,
Amakanji Ekuba, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba
Sc, Juma Luizio, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio
(kulia) akichuana na Beki wa Nakuru All Stars, Amakanji Ekuba, wakati wa
mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye
Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Beki wa Simba, Mwambeleko Jamal
(kushoto) akiwania mpira na beki wa Nakuru All Stars, Nandwa Sosi,
wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea
kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Beki wa Nakuru All Stars,
Mukhwana Sadicky, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa
Simba, Juma Luizio, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super
Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Beki wa Nakuru All Stars, Mukhwana
Sadicky, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Juma
Luizio, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto
(katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Nakuru, wakati wa mchezo wa
mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam

Winga wa Simba, Jamal Mnyate,
(kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Nakuru All Stars, wakati
wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye
Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto,
akijipinda kupiga shuti kuelekea langoni kwa wapinzani, Nakuru All
Stars, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Beki wa Nakuru All Stars, akiokoa
mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Mohamed Ibrahim, wakati
wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye
Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Picha kwa hisani ya Montage Ltd
Mchezo wa pili wa Michuano ya
SportPesa umemalizika kwa Nakuru All Stars kuibuka na ushindi wa jumla
ya Penalti 5-4 mchezo uliomalizika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es
salaam.
Kwa matokeo hayo timu ya Nakuru
inayocheza Ligi daraja la kwanza nchini Kenya imetinga hatua ya Nusu
Fainali ambapo watakutana na Goria Mahia toka Kenya waliofuzu baada ya
kuwafunga Jang’ombe boys Jumla ya mabao 2-0.
Michuano hiyo itaendelea siku ya
Alhamis kwa mechi mbili kupigwa mchezo wa Mapema utawakutanisha mabingwa
wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga watakaocheza na AFS Leorpads na ya pili
itakuwa kati ya Goria Mahia na Nakuru pia ya Kenya kwa hiyo Kenya
wameingiza timu tatu kwenye Nusu Fainali na bingwa wa Michuano atacheza
na Everton ya Uingereza July 13 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam
0 comments:
Post a Comment