By
-
Hii inaweza kupunguza matumani ya mashabiki wa Manchester United kumnunua Antoine Griezman ambaye wamekuwa wakimtafuta kwa muda mrefu na alionekana kabisa huenda akajiunga nao.
Antoine Griezman inasemekana amesaini mkataba mpya katika klabu ya Atletico Madrid ambapo mkataba huo unamfunga hadi mwaka 2022 habari ambazo hazijathibitishwa rasmi na klabu ya Atletico Madrid lakini zimekuwa zikiandikwa sana nchini Hispania.
Mkataba mpya wa Griezman utamfanya mchezaji huyo kiasi cha euro 235,000 kila mwisho wa wiki lakini bado habari njema kwa mashabiki wa United ni kwamba kipengele cha kumuuza Griezman pesa haijapanda na inabaki ile ile euro 88m kama wakimtaka.
Atletico Madrid wanajaribu kuwabakisha wachezaji wao wakubwa wasiondoke katika klabu hiyo kwani wamezuiliwa kufanya usajili baada ya kujaribu kukiuka sheria za wachezaji chini ya miaka 18 na hii inawalazimu kufanya juhudi za kutouza wachezaji wao.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

0 comments:
Post a Comment