Monday, July 24, 2017

CHELSEA CAHILLMENEJA wa Chelsea Mabingwa wa England, Antonio Conte, amethibitisha kuwa Gary Cahill ndie Kepteni wao mpya kuchukua nafasi iliyoachwa na mstaafu John Terry.
Terry alishika Unahodha tangu 2004 hadi alipoondoka Chelsea mwishoni mwa Mwezi uliokwisha baada kumaliza Mkataba wake.
Msimu uliopita, mara nyingi Cahill alivishwa Utepe wa Unahodha kwa vile Terry alikuwa hana namba ya kudumu Kikosini.
Wengi walitarajia Cahill ndie atakuwa mrithi wa Terry lakini David Luiz na Cesar Azpilicueta pia walitajwa kuwa na uwezo wa kuchukua wadhifa huo.
Licha kusisitiza Cahill ndie Kepteni, Conte amewataka Wachezaji wake wote wengine Kikosini kudhihirisha wao pia ni Makepteni.
Ameeleza: "Nadhani tunao Makepteni wengine na wanaweza kuwa Azpilicueta, Luiz, na baadae inaweza kuwa Thibaut Courtois, Cesc Fabregas!"

0 comments:

Post a Comment