KIUNGO
mshambuliaji wa Real Madrid, James Rodriguez amesaini mkataba wa miaka
miwili kujiunga na Bayern Munich kwa mkopo ambako anakwenda kuungana na
kocha wake wa zamani, Mtaliano Carlo Ancelotti.
Rodriguez
atafanyiwa vipimo vya afya na vigogo hao wa Ujerumani kabla ya
kukamilisha uhamisho wake kwenda Allianz Arena - katika dili ambalo
litagharimu hadi Pauni Milioni 40.
Bayern
pia itakuwa na nafasi ya kumnunua moja kwa moja mshambuliaji huyo wa
kimataifa wa Colombia mwishoni mwa mkopo huo Juni 30, mwaka 2019.
Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, James Rodriguez amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Bayern Munich PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mkataba
wa sasa wa mkopo unagharimu Pauni Milioni 9 na Pauni Milioni 31
nyingine zitaongezwa iwapo mwishowe watataka kumnunua moja kwa moja
mchezaji huyo.
Atakuwemo
kwenye kikosi cha Bayern ambacho Jumapili jioni kitakwenda kwenye
michuano ya siku 12 ya Audi Summer Tour nchi za China na Singapore.
Mwenyekiti
wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge ameelezea furaha yake baada ya kumpata
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akisema kwamba alikuwa chaguo kuu
la Ancelotti katika dirisha hili.
Ancelotti
na Rodriguez walifanya kazi pamoja Real Madrid baada ya mchezaji huyo
kujiunga na timu hiyo kwa dau la Pauni Milioni 63 mwaka 2014.
Katika
msimu wao mmoja wa kufanya kazi pamoja Jiji Kuu la Hispania, walishinda
mataji mawili ya UEFA Super Cup na Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
Pamoja na hayo, kufuatia kufukuzwa kwa Ancelotti mwaka 2015 - umuhimu wa Rodriguez ukaanza kupungua Uwanja wa Santiago Bernabeu.
0 comments:
Post a Comment