Wednesday, July 19, 2017


=JUMAMOSI KUIVAA ARSENAL!
CHELSEA SAFARIKIKOSI cha Mabingwa wa England Chelsea kimepaa kwenda Ziarani China na Singapore bila Mastaa wao Wanne lakini kina Chipukizi Wanne huku pia Meneja Antonio Conte akitoa nafasi kwa Straika aliesahaulika Loic Remy.
Asubuhi hii, Chelsea wametua salama huko China.
Mastaa ambao hawamo kwenye msafara ni Majeruhi Eden Hazard na Mchezaji Mpya Tiemoue Bakayoko.
Wengine ambao hawamo Kikosini wakihusishwa na kuhama ni Diego Costa, Nemanja Matic na Kurt Zouma.
Mwingine ambae hayumo Kikosini ni Mchezaji Mpya Antonio Rudiger ambae bado yupo Vakesheni baada kuitumikia Germany kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara.
Kikosini wamo Chipukizi Wanne ambao ni Jake Clarke-Salter, Fikayo Tomori, Marcin Bulka na Kyle Scott.
Pia yumo Straika wao mwenye Miaka 30 Loic Remy ambae hajasikika kwa muda mrefu sasa.
CHELSEA - Kikosi Ziarani: 
Makipa: Thibaut Courtois, Willy Caballero, Eduardo, Marcin Bulka
Mabeki: Cesar Azpilicueta, Gary Cahill, David Luiz, Andreas Christensen, Tomas Kalas, Jake Clarke-Salter, Fikayo Tomori, Marcos Alonso, Kenedy
Viungo: Cesc Fabregas, N'Golo Kante, Mario Pasalic, Lewis Baker, Kyle Scott, Pedro, Willian, Victor Moses
Mafowadi: Charly Musonda, Jeremie Boga, Michy Batshuayi, Loic Remy
MECHI ZAO:
Julai 22 - Arsenal, 1440pm, Bird's Nest Stadium, Beijing
Julai 25 - Bayern Munich, 1435pm, National Stadium, Singapore
Julai 29 - Inter Milan, 1435pm, National Stadium, Singapore

0 comments:

Post a Comment