Tuesday, July 25, 2017

Romelu Lukaku amesema anataka kutengeneza 'Historia yake mwenyewe' huko Manchester United.

MANUNITED LUKAKU MOTOLukaku, Straika kutoka Belgium mwenye Umri wa Miaka 24, alijiunga na Man United mapema Mwezi huu na tayari ashaifungia Bao 2 katika Mechi zao za kujipima wakiwa Ziarani huko USA.
Msimu uliopita, akiwa na Everton, alifunga Bao 25 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Lukaku ndie Mchezaji wa kwanza kutoka nje ya England kufunga Bao 80 kwenye EPL kabla hajatimiza Miaka 24.
Ametamka: "Mie sijakamilika..Nina kazi kubwa ya kufanya lakini upo uwezekano nikawa bora kupita sasa."
Hivi sasa, huko Man United, ameungana tena na Jose Mourinho ambae alikuwa Meneja wa Chelsea wakati Staa huyo anauzwa Julai 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 28 kwa Everton.
Wiki iliyopita Mourinho aliulizwa anawafananisha vipi Lukaku na Didier Drogba alieifungia Chelsea Bao 157 katika Mechi 341 na kutwaa EPL mara 3 na UEFA CHAMPIONZ wakati Mourinho ni Meneja huko Stamford Bridge.
Mourinho alijibu: "Sifananishi. Sifananishi hata kidogo. Mmoja ana Historia yake na mwingine ndio kwanza anaianza Historia yake!"
Nae Lukaku amesema yeye na Drogba wako tofauti kabisa.
Akiongea na BBC Sport, Lukaku ameeleza: "Drogba ni Mchezaji anaehodhi Mpira, anaelengwa katika kushambulia. Mie napenda kuwa na Mpira miguuni na kukimbia kupenya nyuma ya Difensi!"
Ameongeza: "Mimi ni Romelu Lukaku, nataka kutengeneza Historia yangu mwenyewe!"
Kuhusu kuichagua Man United badala ya Chelsea ambayo pia ilitoa Ofa sawa, Lukaku amesema kuwa maono ya Mourinho ndiyo yaliyomfanya aamue kujiunga na Man United.
Amesema: "Mazungumzo yangu na Meneja yalinipa uhakika zaidi. Alinieleza mipango yake na jinsi anavyotaka kuijenga Klabu na kutaka mie niwe sehemu ya mipango hiyo. Yeye ni Meneja ambae daima aliniamini na mie naamini kazi zake. Itakuwa ni safi sana kufanya nae kazi."
Ameongeza: "Mie nimekuwa nikifanya kazi tangu nina Miaka 11!"
Lukaku alikuwa na Miaka 16 tu na bado yuko Skuli alipoanza kucheza Mechi yake ya kwanza kama Profeshenali akiwa na Klabu ya Belgium Anderlecht.
Mwaka Mmoja baadae akawa ndio Mfungaji Bora wa Ligi na kutwaa Ubingwa.
Lukaku alijiunga na Chelsea akiwa na Miaka 18 na kuichezea Mechi 15 tu na kisha kupelekwa kwa Mkopo huko Everton.
Miaka Mitano baadae Lukaku ameweka Historia ya kuwa Mchezaji wa 5 wa Bei Ghali Duniani na aliefunga si chini ya Bao 15 za EPL kila Msimu katika Misimu Mitano iliyopita.
Ameeleza: "Nilifanya kazi niwe Pro tangu nina Miaka 11. Daima nimekuwa na lengo la kutwaa Makombe mengi na kuichezea Klabu kama Manchester United! Nataka niikamate fursa hii!"
LUKAKU - TAKWIMU ZAKE:
-Alipopiga Bao 2 Mwezi Machi, aliweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza wa Everton tangu Gary Lineker Mwaka 1985/86 kufunga Bao 20 katika Msimu mmoja.
-Yeye ni Mchezaji wa 4 kufunga Bao 80 za EPL kabla kufikia Miaka 24 na wengine ni Wachezaji wa Kimataifa wa England Michael Owen, Robbie Fowler na Wayne Rooney.
-Lukaku ndie alieifungia Everton Bao nyingi kwenye EPL, Bao 68, katika Historia ya Klabu hiyo.
- Yeye ni mmoja wa Wachezaji Watatu waliofunga zaidi ya Bao 10 kila Msimu katika Misimu Mitano iliyopita ya EPL. Wengine ni Sergio Aguero na Olivier Giroud.
 

0 comments:

Post a Comment