Thursday, October 5, 2017

Ni kweli nilipokuwa Yanga sikupata nafasi ya kucheza kama nilivyotarajia. Mwanzoni nilikuwa napata nafasi lakini baada ya kuondoka aliyekuwa kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa kwenda kuifundisha timu ya taifa kila kitu kikabadilika kuanzania hapo.
Kuondoka kwa Mkwasa ndani ya Yanga kulibadili kila kitu kwenye timu kwa upande wangu, nikawa sichezi na thamani yangu ikashuka kwenye kikosi.
Mambo yalilivyokuwa chini ya utawala wa Hans van Pluijm 
Kuna mambo mengi sana juu ya hilo, siwezi kusema kila kitu kilichokuwa kinatokea lakini kuna watu wanajua ukweli wote. Kuna chuki  zikaanza kupandikizwa na baadhi ya watu juu yangu kwa hiyo siwezi kuanza kutaja watu kwa majina lakini wao wanajijua.
Je ubora wa wachezaji wengine kwenye nafasi yake ulikuwa kikwazo kwake?
Sio kweli na siamini katika hilo, mimi najiamini ni mchezaji mzuri ndio maana waliamua kunisajili kwenye timu yao kuhusu suala la kushindwa kupata nafasi kwa sababu ya uwepo wa wachezaji fulani kwangu halipo, kwa sababu kuna wakati nilikuwa nacheza na kufanya vizuri.
Kutoonekana kwenye timu kwa muda mrefu
Lengo la kila mchezaji kwenye kila timu ni kupata nafasi ya kucheza na kuonekana, sasa kama huchezi na hupati nafasi maana yake nini? Unaishia kufanya mazoezi halafu hupangwi hata kwenye benchi la wachezaji wa akiba haupo inashusha morali yako kiuchezaji.
Kuna wakati kuna timu zilikuwa zinakuja zinataka kunisajili lakini kuna viongozi walikuwa wanakataa kuniruhusu niondoke ndio maana niliamua kukaa nikasubiri hadi mkataba wangu ulipomalizika nikaondoka. Sasa hivi nipo kwenye klabu ambayo naamini nitafanya vizuri kwa sababu mchezaji anaweza kufanikiwa popote ili mradi anaonesha uwezo wake haijalishi ni timu gani.
Ujio wa Lwandamina haukubalidili kitu
Kama nilivyosema mwanzo, nilikuwa sichezi sio kwa sababu sina uwezo kuna mambo mengi sana hapa, mengine sio poa kuyaanika hadharani nabaki nayo mimi mwenyee lakini kuna watu walikuwa wanapandikiza chuki ili mimi nisipate nafasi ya kucheza Yanga.
Kwa hiyo ujio wa kocha mpya haukubadili chochote kwa upande wangu, ndio maana niliendelea kubaki nje ya timu.
Malengo hayakutimia Yanga
Nikiwa Yanga malengo yangu hayakutimia, nilienda pale nikiwa na malengo ya kucheza na kuonekana lakini hilo halikuwezekana. Hayo ndio maisha ya mpira unaweza ukashindwa kutimiza malengo sehemu lakini yakatimia ukiwa sehemu nyingine ndio maana nipo Lipuli ambako nina amani na nadhani nipo sehemu sahihi kwa ajili ya kutimiza kile kilichoshindikana semu nyingine.

0 comments:

Post a Comment