Kipa wa Manchester City, Claudio Bravo akishangilia baada ya kuokoa penalti za Jamie
Vardy na Riyad Mahrez wa Leicester City na kuipa timu yake ushindi wa
penalti 4-3 hivyo kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu
kama Carabao Cup kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120. Waliofunga
penalti za City ni İlkay Gundogan, Yaya Toure, Lukas Nmecha na Gaabriel Jesus wakati waliofunga za Leicester ni Christian Fuchs, Harry Maguire na Vicente Iborra.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa King Power, Bernardo Silva alianza kuifungia City dakika ya 26 kabla ya Vardy kuisawazishia Leicester kwa penalti dakika ya saba ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90

0 comments:
Post a Comment