LIGI Kuu Bara inatarajiwa kuendelea tena
wikiendi hii na timu shiriki zinapaswa zijipange kwelikweli kwani winga
ghali zaidi nchini, Shiza Kichuya ametamba atakuja kivingine na kutisha
zaidi katika ligi hiyo.
Kichuya anayeongoza kwa kuifungia Simba
mabao mengi zaidi tangu msimu uliopita (17) alisema; “Simba tuna raha
kukaa kileleni na bila shaka mashabiki wetu watakuwa wana furaha mtaani,
hilo linawafanya wapinzani wetu, waumize akili namna ya kurejea kwa
kishindo,” alisema.
Kichuya alisema hilo litaleta changamoto
kwa wachezaji kutaka kuonyesha ufundi wao na ukubwa wa majina yao mbele
ya mashabiki wa timu zao, kitu alichokiona kama kinaongeza umakini wa
kazi zao.
“Mchezaji mwenye malengo lazima ajipange
na kujiuliza alifanya nini wakati ligi inachezwa na sasa anapaswa kuwa
na jipya gani la kusaidia kutimiza malengo yao timu.”
“Nataka Simba ichukue ubingwa, hilo
linanifanya niendelee kupambana kuhakikisha ndoto inatimia na kuweka
rekodi ya kukumbukwa na vizazi vijavyo,” alisema nyota huyo wa zamani wa
Mtibwa Sugar.

0 comments:
Post a Comment