Manchester United
haitashindana na Barcelona katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa
Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Antoine Griezmann. (Marca)
Paris
St-Germain wanachunguza hali ya Marouane Fellaini katika uwanja wa Old
Trafford na wako tayari kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30
katika uhamisho wa bure msimu ujao.(Daily Mirror)Liverpool ilimsafirisha daktari wake ili kuchunguza hali ya kimatibabu ya beki wa Southampton , 26, Virgil van Dijk ili kuweza kukamilisha usajili wa dau la £75m haraka iwezekanavyo - kabla ya Mancity kuwa na hamu ya mchezaji huyo.(Liverpool Echo)

Chelsea ilifeli katika harakati za kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Ubelgiji msimu uliopita lakini inaweza kuwasilisha ombi jingine. (Sun)
West Ham United inakaribia kumsajili beki wa Swansea mwenye umri wa miaka 23 Alfie Mawson. (ESPN)

Everton inalenga kumsajili mshambuliaji wa Besiktas Cenk Tosun, 26, mwezi Januari na inaweza kulipa £20m kumnunua mchezaji huyo wa timu ya taifa la Uturuki. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa zamani wa Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal anatathminiwa kuchukua ukufunzi wa klabu ya Swansea. (Sun)
Birmingham ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Nigeria mwenye umri wa miaka ,24, Shehu Abdullahi kutoka klabu ya Cypriot Anorthosis Famagusta. (Birmingham Mail)
Crystal Palace, Everton na Burnley zina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 24 Karl Toko Ekambi. (France Football - in French)

Norwich iko tayari kumsajili kiungo wa kati na mshambuliaji wa Lyon ,21, Aldo Kalulu, ambaye amekuwa katika mkopo katika klabu ya Sochaux. (France Football - in French)
Mshambuliaji wa Newcastle mwenye umri wa miaka 23 Aleksandar Mitrovic anataka kuondoka katika klabu hiyo. (Daily Mirror)

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA lina imani kwamba Uingereza itakuwa miongoni mwa mataifa yatakayopigiwa upatu kuandaa kombe la dunia la mwaka 2030. (Sun)
Mshambuliaji wa Uruguay Sebastian Abreu, 41, ameweka rekodi mpya ya dunia kwa kujiunga na klabu ya 26 tangu aanze kucheza soka. (Daily Mail)
Mkufunzi wa West Ham David Moyes amesema kuwa hatua ya kumsaidia mshambuliaji Marko Arnautovic kujiimarisha ilikuwa sawa na kumwambia kwamba hatocheza iwapo hataki kukimbia (Evening Standard)

0 comments:
Post a Comment