Southampton inataka
kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Uingereza Daniel Sturridge, 28,
kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Telegraph)
Klabu hiyo pia
inataka kutumia fedha zake ilizopata baada ya kumnunua beki wa Uholanzi
Virgil van Dijk's ili kumrudisha mshambuliji wa Arsenal Theo Walcott.
(Mirror)
Manchester United na Tottenham pia zina hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 (AS via Talksport)

Arsenal inajiandaa kumnunua winga wa Algeria na Leicester Riyad Mahrez, 26, huku mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo (Le Buteur - in French)
Manchester City itataka kumsajili beki wa kati wa West Brom na Ireland kaskazini Jonny Evans, 29, ama beki wa Real Sociedad Inigo Martinez mwezi Januari. (Telegraph)

United imesema kuwa iko tayari kumuachilia kiungo wa kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 28, katika mpango huo.(Sun)
West Ham iko tayari kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Andre Schurrle, 27, kwa mkopo mwezi Januari. (Guardian)

Wolfsburg inataka kumsajili kwa mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na klabu hiyo ya Bundesliga kwa mkopo mwezi August. (ESPN)
Stoke inataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Danny Ings, 25, kwa mkopo , lakini itakabiliwa na ushindani kutoka kwa Newcastle, West Ham na West Brom. (Independent)

0 comments:
Post a Comment