Mkufunzi wa
Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wakati wa
Arsenal na Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 Mesut Ozil. (Telegraph)
Liverpool
wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Brazil, 25, Philippe Coutinho kwa
Barcelona mwezi Januari, lakini iwapo klabu hiyo itatoa dau la £127m.
(Mundo Deportivo - in Spanish)Mshambuiaji wa Inter Milan raia wa Argentina Mauro Icardi, 24, ana thamani ya Yuro 200m kulingana na ajenti wa mchezaji huyo. (Corriere dello Sport, via BeInSport)

Real Madrid wamezuia usajili wa dau la £38m wa Vinicius Junior na wameamua kumuacha katika klabu yake ya Brazil ,Flamengo kwa msimu mwengine huku kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mechi za maandalizi ya msimu ujao mwaka ujao (AS)
Tottenham imekataa kuongeza mishahara ya wachezaji wake licha ya hofu kwamba mazungumzo ya kuongeza kandarasi yamekwama kati ya timu hiyo na beki wa ubelgiji Toby Alderweireld. (Daily Mail)

Mkufunzi wa klabu ya Bournemouth Eddie Howe atafanya mazungumzo na mshambuliaji wa klabu hiyo Lewis Grabban, 29, ambaye yuko katika klabu ya Sunderland kwa mkopo (Bournemouth Echo)

Winga wa Leicester Riyad Mahrez anasema kuwa uwezekano wa yeye kujiunga na Arsenal msimu ujao uko asilimia 50. (Daily Mail)

Beki wa Liverpool Joel Matip, 26, huenda akauguza jeraha la nyonga kwa hadi mwezi mmoja (Telegraph)
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anatarajia kwamba atapata makaribisho mema kutoka kwa mashabiki wa Chelsea wakati atakaporudi katika uwanja wa Stamford Bridge, ambapo alikuwa kaimu mkufunzi siku ya Jumamosi. (Daily Mail)
Mkufunzi wa Ubelgiji amesema kuwa familia yake itakuwa ikiunga mkono Uingereza wakati timu hizo mbili zitakapokutana katika kombe la dunia la mwaka ujao.(Mirror)
0 comments:
Post a Comment