Katika hali isiyotarajiwa, nyota wa zamani wa timu ya taifa Nigeria Wilson Oruma amepata ugonjwa wa akili (uchizi) baada ya kile kinachotajwa kwamba alizulumiwa pesa na mchungaji.
Inadaiwa
kwamba Oruma aliambiwa na mchungaji huyo atoe kiasi cha Naira 1.2B kwa
ajili ya kuanzisha biashara ya mafuta ambayo angekuwa sehemu ya biashara
hiyo lakini mambo yalibadilika.Rafiki wa karibu wa Oruma aitwaye Emakpor Dibofun amesema baada ya nyota huyo kuzulumiwa kiasi hicho cha pesa amekuwa akihangaika kutafuta msaada wa kupata pesa hiyo lakini ilishindikana.
Hali
hiyo ilianza kumpa msongo wa mawazo Orum na tariibu akaanza
kuchanganyikiwa na sasa hali yake imeanza kuwa mbaya zaidi huku
muonekano wake ukibadilika kabisa na kuanza kuongea vitu vya ajabu.Mlinzi mmoja katika ofisi mjini Lagos amesema Oruma anatia huruma na hali yake inawafanya watu wengi wasikumbuke kwamba ni yeye huku akitembea na kuongea peke yake mji mzima wa Lagos.
Oruma amewahi kuichezea Super Eagles akiwa pamoja na Nwanko Kanu na Jay Jay Okocha lakini pia mchezaji huyo pia alikuwepo katika kikosi cha Nigeria U-17 ambacho kilibeba kombe la dunia 1993.

0 comments:
Post a Comment