Na Priva ABIUD
Sio jambo la kushangaza Mesut Ozil kuongeza mkataba. Ozil alikuwa na nafasi kubwa ya kuondoka dirisha dogo. Lakini kufikia sasa ni ngumu kuondoka tena. Zipo sababu ambazo kwa mtazamo wangu mimi zinamfanya asiondoke.
Dili la Sanchez
Mourinho
alitaka kumpeleka Ozil Old Trafford. Ozil aliwahi kufanya kazi na Jose
Mourinho wakiwa wote ndani ya klabu ya Real Madrid. Dili la Sanchez
kwenda Uninted limetibua mipango. Sanchez alihitajika na Man city lakini
amebadili gia angani. Man united haiwezi kumnasa tena Ozil na Sanchez
kwa wakati mmoja, ni sawa na Magu na JK kwenda UKAWA wote kwa pamoja.
Bila shaka Wenger hawezi kumuozesha mwanae wa kike pia akampa na mkwe
Ng’ombe badala ya yeye kupokea mahari (Mkhitaryan).Ujio wa Majina mapya
Hii
ni Kamari kwa Mesut Ozil. Wenger amethibitisha ujio wa majina mapya.
Arsenal inaweza isipate mafanikio makubwa lakini bado wana nafasi ya
kushiriki michuano mikubwa na midogo. Malcom raia kutoka Brazil, Piere
Aubemeyang kutoka Borussia Dotmund pamoja na Henrik Mkhitaryan kutoka
Manchester United ni majina yaaliyopo kwenye notibuku ya wenger. Kwa
akili ya haraka haraka kikosi cha arsenal kitaimarika sana hasa baada ya
Chamberlain, walcot pamoja na sanchez kuondoka. Bali hiku litampa
hamasa mpya Mesut Ozil kubaki.Haoni pakwenda na hahitajiki sana
Ozil ni mchezaji wa kiwango cha juu. Ni moja kati ya viungo mahiri sana katika robo ya eneo la timu pinzani. Shida ni kasi yake ya uchezaji. Ni makocha wachache wanaoweza kumvumilia.
Ni
mchezaji ambaye tayari ameshacheza klabu kubwa kama Real Madrid. Mbaya
Zaidi katika umri wake wa miaka 29 bado yupo kwenye kiwango salama. Ana
kiwango bora bado, lakini ni timu gani ipo tayari kutoa ada ya kumnunua
na kumlipa maslahi anayotaka katika umri wake huu? Ozil anafahamu fika
kiwango chake bado hakijshuka, na anahitaji timu itakayokidhi maslahi
yake. Je ni vilabu vingapi ambavyo vinaweza kumlipa? labda avuke bara
aende uchinani au Marekani. Je katika hivo vilabu vinavyoweza kumlipa
kuna uhakika wa nafasi? Je vinahitaji huduma yake?. Kwa haraka haraka
timu nazoziona ni kama PSG, Man United Man City, Barca na Buyern. Lakini
wote hao wana wachezaji sahihi kwenye eneo Ozil analocheza.Mimi nadhani Ozil anapaswa kumlaumu Sanchez aliyeenda kuchukua nafasi yake Old traford. Amepokonywa tonge hivyo apambane na sahani yake akomboleze mchuzi alioacha sanchez. Na Uzuri ni kwamba Muonekano wa Ozil n mpole, nadhani Wenger hashindwi kumbebeleza na akabaki.

0 comments:
Post a Comment