
Liverpool wako tayari kufanya hima kujaza pengo lilioachwa na Philippe Coutinho ambaye ameelekea Barcelona huku wing'a wa Monaco Thomas Lemar 22, akiwa nambari moja katika orodha yao.

Ciy pia wanamwinda mlinzi wa Leicester Harry Maguire, 24, na wanaweza kutoa ofa ya pauni milioni 50 kwa kiungo huyo wa kati wa zamani wa Hull City. (Sun on Sunday)
Manchester United huenda wakajaribu kumleta Gareth Bale kutoka Real Madrid, kabla ya msimu wa kununua wachezaji wapya kukamilika. (Sunday Express)

Meneja Mauricio Pellegrino anasema Southampton wana matumaini ta kumsaini wing'a wa Arsenal na England Theo Walcott, 28. (ESPN)
Meneja wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amekana madai ya kumuuza kiungo wa kati raia wa Chile Arturo Vidal kwenda Chelsea mwezi Januari (Mail on Sunday)
0 comments:
Post a Comment