

Hii ni game ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kukutanisha timu zenye mashabiki wengi England na Afrika kwa ujumla, Man United wakiwa nyumbani licha ya kuanza kuruhusu goli lakini walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Romelu Lukaku dakika ya 39, Jesse Lingard dakika ya 75 wakati goli pekee la Chelsea lilipatikana dakika ya 32 kupitia kwa Willian.

Ushindi huo sasa unaifanya Man United kufikisha jumla ya point 59 na kuwa nafasi ya pili nyuma ya Man City inayoongoza Ligi kwa tofauti ya point 13, Chelsea wao baada ya kupoteza leo wameshuka hadi nafasi ya 5 kwa kuendelea kusalia na point 53, hivyo kutokana na Spurs kushinda wao wamesogea nafasi ya 6 kwa kuwa na point 55.
0 comments:
Post a Comment