Chelsea inakabiliwa
na ushindani mkali kutoka kwa Bayern Munich katika kumsajili kiungo wa
kati wa Borussia Dortmund Christian Pulisic. (Mail)
West Ham iko
tayari kumpatia David Moyes mkataba wa miaka miwili mwisho wa msimu huu
iwapo atawasaidia The Hammers katika ligi ya Uingereza na raia huyo wa
Uskochi tayari anatafuta wachezaji wa kuwasajili msimu ujao(Express)
- Mourinho: Man United waliwadhibiti Chelsea
- Chelsea waafikiana kumnunua Morata
- Mikel atangaza kuihama Chelsea

Mkufunzi wa zamani wa Watford Marco Silva ndio anayepigiwa upatu kumrithi Alan Pardew iwapo atandoka West Brom(Birmingham Mail)

Crystal Palace imejiandaa kumsaini kipa wa zamani wa Liverpool na Brazil Diego Cavalieri katika uhamisho wa bure(ESPN)
Liverpool inajiandaa kumsajili kinda wa Lyon na Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Mohamed Bahlouli. (France Football via Sun)
Lengo la kocha Jurgen Klopp la kumsajili kipa wa Roma Alisson imepigwa jeki baada ya klabu hiyo ya Itali kupata kipa atakayechukua mahala pake (Gianluca di Marzio via Sun)

Afisa anayesaka wachezaji katika klabu ya Chelsea Eddie Newton amefichua kwamba amemkagua mshambuliaji wa Everton na Uturuki Cenk Tosun, 26, na anamtarajia kufanya vyema katika klabu hiyo. (Liverpool Echo)
Philippe Coutinho alikuwa na wakati mgumu katika kipindi cha saa 24 zilizopita mjini Barcelona baada ya gari lake kuvutwa kwa kuliegesha katika eneo lisilofaa na baadaye nyumba yake ikavunjwa na kuibiwa. (Daily Mail)
0 comments:
Post a Comment