Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa
anawapa Simba nafasi ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, endapo
watapambana zaidi huku akisema bado ni timu ya kawaida mno.
Akilimali ameeleza kuwa, Simba imekuwa ikifanya vizuri msimu huu tofauti
na miaka ya nyuma, lakini bado anaiona ya kawaida kwa kusema endapo
watapoteza baadhi ya mechi zijazo, basi nafasi hiyo hawana.
Akilimali ametamba kuwa wao watapambana kwa kila liwezekanalo waweze
kuzidi kuutetea ubingwa kwa tofauti ya pointi na si magoli, kutokana na
watani wao kuwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga mpaka sasa.
Mpaka sasa Simba ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi, katika michezo 19 iliyocheza msimu huu.
Simba hivi sasa wako katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo ujao wa
ligi dhidi ya Stand United ya SHinyanga utakaochezwa Ijumaa ya wiki hii.
0 comments:
Post a Comment