Manchester City
wanampango wa kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard,27, kwa
mkataba wa £100m baada ya meneja Pep Guardiola kumuweka mchezaji huyo
kuwa kiungo muhimu anayemlenga wakati wa uhamisho.(Star)
Klabu ya
Utaliano ya AC Milan imempatia kiungo wa kati wa Manchester United
Marouane Fellaini,30, mkataba wa miaka mitatu huku kiungo huyo raia wa
Ubelgiji kuwa huru kwa uhamisho wa bure katika majira ya joto. (Times -
subscription required)Conte: Nitamsalimia Mourinho kwa mkono
Beki wa Tottenham,Toby Alderweireld, 29, ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuuzwa na klabu ya United wakati wa uhamisho wa majira ya joto. (Mirror)
West Ham inaamini kumteuwa Manuel Pellegrini kama meneja wao mpya wiki hii- ambayo itaipatia nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati Yaya Toure, 35, aliyeiaga Manchester City. (Telegraph)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anatarajiwa kuiaga Chelsea kwa saa 48 zijazo - huku meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo. (Express)

Manchester United wavuna zaidi ya Manchester City EPL
Manchester United imekubaliana katika hatua za kwanza na kiungo wa kati kutoka Brazil Talisca, 24 ambaye amekuwa kwenye mkopo na Besiktas kutoka Benfica. (Star)
Uteuzi wa Kocha wa zamani wa Paris St-Germain Unai Emery umewashangaza wengi baada ya kuteuliwa katika dakika za mwisho kuwa meneja mpya wa Arsenal. (Mail)

Mazungumzo ya Napoli na meneja wao Maurizio Sarri yametibuka kutokana na mataminio ya meneja huyo kutaka kuihamia Chelsea. (Mirror)
Mhispania Santi Cazorla ,33, amepewa nafasi ya kujiunga na klabu yake ya zamani ya Villarreal huku mkataba wake na Arsenal ukitarajiwa kukamilika. (Evening Standard)

Beki Partick Thistle Niall Keown, 23, anatarajiwa kubadili majukumu yake kutoka Republic hadi Kaskazini mwa Ireland - na meneja Michael O'Neill anataka kumsajili kiungo wa kati wa Klabu ya QPR Sean Goss, 22, kwa mkopo. (Daily Record)

0 comments:
Post a Comment