Wakati
pambano la mechi ya Ligi Kuu huko Mtwara kati ya Ndanda FC dhidi ya
Simba likusubiriwa kwa hamu, unaambiwa mwitikio wa mashabiki umekuwa
mkubwa.
Foleni
kubwa ya mashabiki wa timu hizo mbili huku wageni ambao ni Simba
wakionekana kuleta hamasa kubwa katika dimba la Nangwanda Sijaona
wameanza kumiminika ndani ya Uwanja huo.
Mashabiki
hao wamejitokeza kwa wingi katika uwanja huo ili kuweza kushuhuia mechi
hiyo ambayo ina motisha ya aina yake leo Jumamosi.
Simna
inakutana na Ndanda ikiwa na rekodi ya kutopoteza alama tatu tangu
walima korosho hao wapande daraja kushiriki Ligi Kuu Bara mwaka 2014.
Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni ambapo itakuwa mbashara kupitia kituo cha Azam TV.
0 comments:
Post a Comment