
Barcelona
wamesitisha jaribio lao la kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa
Brazil Neymarkutoka Paris Saint-Germain hadi msimu ujao. (ESPN)
Mazungumzo
kati ya vilabu hivyo yalivunjika baada ya PSG kulegeza masharti yao
licha ya Neymar kujitolea kulipa £17.7m kufikia makubaliano ya usajili
wake. (Sky Sports)- Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 01.09.2019
- Ronaldo amualika Messi mlo wa jioni
- Champions League: Samatta apangiwa mabingwa Liverpool
Roma wanamatumaini ya kusaini kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan ,30. (Sky Italy - in Italian)

Mshambuliaji wa Frankfurt mwenye umri wa miaka 25 Mcroatia Ante Rebic anajiandaa kujiunga na AC Milan, huku mshambuliaji Andre Silva, 23 Mreno akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo. (Goal)
Kipa wa Paris St-Germain Alphonso Areola, 26, anatarajiwa kumilisha uhamisho wake kwenda Real Madrid siku ya mwisho katika mkataba ambao utamwezesha kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 32, kujiunga na klabu hiyo. (Mirror)

Mlinzi wa Bayern Munich Mjerumani Jerome Boateng, 30, anakaribia kujiunga na mabingwa wa Italia uventus. (Bild, in German)
Juventus bado wana matumaini ya kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona wa miaka 31 Mcroatia Ivan Rakitic - na huenda wakatoa ofa ya kumuachilia mchezaji wa kiungo cha kati Mjerumani Emre Can, 25, kama sehemu ya kufikia mkataba wa kumsajili Ivan Rakitic. (Sport - in Spanish)

Borussia Dortmund wanapigiwa upatu kumsajili kipa wa Liverpool wa miaka 18 Bobby Duncan ikiwa klabu hiyoo ya Ligi Kuu ya Uingereza ataamua kukomesha mkataba wake . (Mirror)
Tetesi Bora Jumapili
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27 anaweza kukataa kusaini mkataba mpya na Manchester United ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusajiliwa Real Madrid. (Mirror)
Bayern Munich inataka kumsaini winga wa Mancity Leroy Sane licha ya kwamba winga huyo mwenye umri wa miaka 23 atauguza jeraha la muda mrefu(Mirror)
Alexis Sanchez, 30,amejiunga na Inter Milan katika mkataba wa muda mrefu wa mkopo baada ya meneja wa Manchester United, Solskjae kumwambia kuwa mchezaji huyo anaweza kuchezea mashindano ya vikombe na ligi ya ulaya.(Sun)

Mshambuliaji wa West Ham na Javier Hernandez, 31, ametuma maombi yake ya kuhamia Sevilla.(Mail)
Mpango wa Christian Eriksen kutoka Tottenham kwa paundi milioni 72 kwenda PSG imegonga mwamba baada ya Neymarameamua kubaki kwa mabingwa wa ligue 1. (Sun)
0 comments:
Post a Comment