Mchezaji
wa zamani wa Arsenal, Serge Gnabry akishangilia baada ya kufungia
Bayern Munich mabao manne dakika za 53, 55, 83 na 88 katika ushindi wa
7-2 dhidi ya wenyeji Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Kundi B Ligi ya
Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Tottenham Hotspur mjini London.
Mabao mengine ya Bayern Munich yalifungwa na Joshua Kimmich dakika ya 15
na Robert Lewandowski 45 na 87 wakati ya Spurs yalifungwa na Son
Heung-Min dakika ya 12 na Harry Kane kwa penalti dakika ya 61
Home
»
»Unlabelled
» SERGE GNABRY APIGA NNE BAYERN MUNICH YAICHAPA TOTTENHAM 7-2 LONDON
Wednesday, October 2, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment