
Barcelona huenda
ikamjumuisha mshambulizi wa kimataifa wa Ufaransa wa miaka 28, Antoine
Griezmann katika mkataba wa kumsajili tena mshambuliaji nyota wa Brazil
Neymar, 27, kutoka Paris Saint-Germain msimu ujao. (Le10Sport - in
French)
Chelsea inamatumaini kuwa mlinzi wake Fikayo Tomori, 21,
na mshambuliaji Tammy Abraham, 22, watasaini mkataba mpya wiki chache
zijazo. Wachezaji hao wawili wamejumuishwa katika kikosi England cha kufuzu kwa kintang'anyuro cha Euro 2020 baadae mwezi huu. (Standard)
- Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 04.10.2019
- 'Je Man United ilimkosa 'Ronaldo mpya'?
- Klabu ya Nice yamfuta kazi mchezaji aliyeiba saa
Kocha wa Everton Marco Silva amesema mchezaji wa safu ya mashambulizi ya England ya wachezaji wa chini ya miaka-19 -Anthony Gordon, 18, anakaribia kujiunga na kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Liverpool Echo)
West Ham inamnyatia kiungo wa kati wa miaka 20 raia wa Bolivia, Daniel Camacho, ambaye anachezea klabu ya nyumbani ya Aurora. (Diez via Sport Witness)
Real Madrid inapania kumuajiri meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte kama kocha wao mpya baada ya kumfuta kazi Julen LuLutetiu mwaka jana lakini uamuzi huo ukabatilishwa kufuatia ushauri wa nahodha Sergio Ramos.(Fichajes.net via Mail)
Kocha wa Anderlecht, Vincent Kompany anamlenga mlinzi wa Wales Ashley Williams,35, mkataba wake na Bristol City utakapokamilika mwezi Januari. (Sun)
Kiongo wa safu ya mashambulizi ya Croatia, Mario Mandzukic, 33, anayelengwa na Manchester United nu miongoni mwa wachezaji watatu watakaouzwa na Juventus mwezi January. (Calciomercato - in Italian)
Stakabadhi iliyovujishwa umefichua kiwango cha faini Real Madrid inayowatoza Inawatoza wachezaji wake kwa kukiuka sheria kama vile kuchelewa kufika kwa mazoezi nakutumia simu wakiwa katika basi la timu au chumba cha kubadilisha mavazi. (Marca)
0 comments:
Post a Comment