SHOMARI Kapombe,
mchezaji wa Timu ya Taifa anayekipiga timu ya Simba kwa sasa ambao ndio
mabosi wake ameamua kwa hiyari yake yeye mwenyewe kuandika barua kuomba
kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania.
Kwa alichokifanya
sio kitendo kibaya kwa kuwa ni maamuzi yake binafsi na hakuna ambaye
amemlazimisha afanye jambo hilo ni wakati wake kutokana na maamuzi yake.
Hakuna ambaye hajui uwezo wa Kapombe akiwa ndani ya uwanja na kila mmoja kwenye ulimwengu wa mchezo anatambua thamani yake.
Kwa kuwa ameamua
kufanya hivyo basi hapaswi kulaumiwa na wapenzi wa mpira kwa kudai
kwamba ameisha muda wake ili hali bado ni kijana.
Ameandika barua ya
kuomba kustaafu timu ya Taifa hiyo ipo wazi kutokana na dhamira yake
kuona kwamba anahitaji kupumzika kuendelea na mambo yake ambayo
ameyaweka bayana.
Tuheshimu maamuzi
yake kwa kuwa kila mtanzania ana uhuru wa kuongea na kufanya kile
ambacho anaona ni sahihi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.
Ameweka wazi sababu kubwa kuwa ni ile ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara hasa akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania.
Hilo lipo wazi kwani
hata sasa bado anasumbuliwa na majeraha ambayo anayo na ikumbukwe
kwamba mchezaji akiwa anapata majeraha ya mara kwa mara ufanisi wake
unapungua.
Amekuwa hachezi mara
kwa mara akiitwa timu ya Taifa kutokana na kusumbuliwa na majeraha
hivyo ameomba apumzike ili apone majeraha yake.
Amekuwa anasumbuliwa
na majeruhi kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likimfanya ashindwe
kuitumikaia timu ya Taifa kipindi akiitwa.
Wakati wa michuano ya Chan pamoja na ile ya Kufuzu Kombe la Dunia alipata bahati ya kuitwa ndani ya timu ya Taifa.
Tukazungumza naye
mengi kuhusu maisha ya soka na maisha binafsi, kiukweli aliongea mengi
ambayo yanaumiza licha ya kwamba ni mpambanaji kwa sasa.
Alieleza hali halisi
ya muda ambao anautumia kutibu majeraha yake kuwa mkubwa kuliko ule wa
kuwa uwanjani jambo lililomfanya ashindwe kupata muda kuichezea timu ya
Taifa.
Pia
rekodi zinaonyesha kwamba majeraha yake mengi ameyapata timu ya taifa
jambo hilo ndilo ambalo limemsukuma aombe kujiweka pembeni kwa muda.
Tuache kumdharau kwa
maamuzi ambayo ameyafanya kwa sasa jukumu letu ni kuheshimu mawazo yake
na kuendelea kumuombea ili arejee kwenye ubora wake.
Tusimbeze kwa kusema
kuwa hana mchango ndani ya timu ya Taifa ana haki ya kuomba kile
anachokiamini kutokana na hulka yake ya nidhamu.
Hakuna asiyependa
kuitumkia timu ya taifa hasa kwa mzalendo mwenye utu na anayetambua
kwamba ni heshima kuitumikia timu ya Taifa.
Umri wake bado mdogo
unamruhusu kufanya mengi ambayo anayafikiria kwa sasa hivyo basi apewe
nafasi ya kueleza kile kilicho ndani ya moyo wake.
Kwa kukaa kwake nje
kutamfanya arejee kwenye ubora wake na wakati utafika atarejea kwenye
ubora wake na ataomba kurejea kwenye timu ya Taifa.
Ushauri wangu kwa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inapaswa imuandalie mechi ya heshima
kwa ajili ya kumpa sapoti na kutambua mchango wake ndani ya timu.
Kwa kufanya hivyo
kutampa moyo Kapombe wa kuweza kurejea tena wakati afya yake
itakaporejea kwenye ubora wake hasa kutokana na kuendelea kupambania
afya yake.
Ipo siku atarejea kwenye uwanja na kuomba kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania ambayo ni ya kila mmoja kwenye kazi yake.
Wapenda soka
tusisahau kumuombea Kapombe kwa kuwa tunatambua anapenda kuendelea
kuitumikia timu yake ya Taifa ila majeraha ndio kikwazo kwake.
Imani ya wapenda
soka ni kwamba atarejea na atapona majeraha yake ambayo yanamsumbua kwa
sasa jambo litakalokuwa la furaha kwa wapenda soka.

0 comments:
Post a Comment