JURGEN
Klopp, kocha mkuu wa Liverpool amethibitisha kuwa mshambuliaji wake
Mohamed Salah atarejea uwanjani Jumatano kwenye mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Napol.
Salah
raia wa Misri alikosa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal
Palace ambao Liverpool ilishinda mabao 2-1 na kuifanya izidi kujikita
kileleni ikiwa na pointi 37 kwenye msimamo kutokana na kusumbuliwa na
majeruhi.
.
Klopp
amesema kuwa Salah alikuwa fiti kuivaa Crysytal Palace kutokana na hali
yake kuimarika ila aliamua kumpumzisha kwa ajili ya kazi nzito ya
jumatano dhidi ya Napol.
“Salah
yupo vizuri na ilibidi aanze kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace
niliamua nimpe mapumziko ila mwisho wa siku mchezo wetu tulishinda kwani
hakuwa na timu kwa muda wa siku nane alikuwa nchini Misri na mabao
yalifungwa na Robert Firmino na Sadio Mane.
“Tulipaswa
kufanya changuo la kumuanzisha ama kumuacha apumzike tukakubaliana
tumpumzishe atarejea uwanjani Jumatano kukabiliana na Napol,” amesema
Klopp.
0 comments:
Post a Comment