
Paris St-Germain ipo tiyari kupambana na Inter Milan kumuwania kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Mirror)
Mkurugenzi
mtendaji wa Atletico Madrid Maguel Angel Gil Marin, alikuwa jijini
Paris kufanya mazungumzo na PSG kuhusu mshambuliaji wao Edinson Cavani,
32. (Marca)Mshambuliaji wa Arsenal Alexanndre Lacazette, 28, ni pendekezo la Atletico Madrid iwapo hawatampata Cavani. (Sky Sports)
Manchester City imeondoa uwezewekano wa mlinzi wake wa kati Muingereza John Stones, 25, kujiunga na miamba ya London Arsenal katika dirisha hili la usajili. (Manchester Evening News)
Kocha Pep Guardiola hana nia ya kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Manchester United Ed Woodward ameonekana akisafiri kuelekea Ufaransa kwa kutumia treni ya Eurostar, United inapania kumsajili kiungo wa Lile mfaransa Boubakary Soumare, 20. (Star)
United itatakiwa kulipa pauni milioni tano kumfuta kazi Ole Gunnar Solskjaer. (Sun)
Wakala wa winga wa United Mholanzi Tahith Chong, 20, ameonekana Inter Milan huku mchezaji huyo akitarajia kuondoka Old Trafford. (Mirror)

Mashambuliaji wa Los Angeles FC Carlos Vela atamkaribisha mshambuliaji wa Sevilla Javier Hernandez , hata kama mchezaji huyo mwenye miaka 31 atacheza na wapinzani wao LA Galaxy. (ESPN)
Mlinda mlango raia wa Ufilipino Neil Etheridge, 29, hatokuwemo katika kikosi cha Cardiff City kitakachoumana na Carlisle katika mzunguko wa tatu wa kombe la FA huku tetesi za yeye kuhamia Westham zikiendelea kushika kasi.(Wales Online)
Inter Milan inamuwinda mlinzi wa Parma Matteo Darmian, 30 .(Tuttomercatoweb - in Italian)
Mshambuliaji wa zamani Darren Bent ametaka kujumuishwa kwa mlinzi wa kushoto wa Manchester United Brandon Williams, 19 katika michuano Euro 2020. (Talksport)
0 comments:
Post a Comment