SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF), limepokea maombi ya waamuzi saba wanaotaka
kutopangwa kuchezesha baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara kutokana na
presha na uoga wa kuboronga katika kufanya maamuzi.
Ishu
hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya sakata la waamuzi kuboronga
katika baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara zilizochezwa hivi karibuni huku
baadhi yao wao wakikumbana na adhabu.
Katibu
Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema wamepokea maombi hayo, lakini
wakaona hilo siyo suluhisho la kuondoa tatizo na badala yake wana mpango
wa kuwaandalia kozi maalumu itakayowanoa na kuwafanya wawe bora katika
siku za usoni.
Kidao
ameliambia Spoti Xtra kuwa, watawapima waamuzi wote kujua kama wana
matatizo ya kiafya kwani kuna uwezekano wakawa na matatizo ya kutoona
mbali.
“Tumepokea
barua za waamuzi saba wakiomba kutopangwa katika michezo ya ligi, hiyo
inatokana na presha na hofu waliyonayo, lakini kutokana na maazimio
yaliyotolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia, tumeamua kuanzisha program
maalumu ya kuwajengea uwezo wa ndani na nje ya nchi waamuzi wote, ambapo
tutawapima afya, ikiwa kuwachunguza kama watakuwa na matatizo ya
kutoona mbali.
“Lakini
pia tutawachunguza wakufunzi wao ili kuona kama uwezo wao unakidhi
kiwango cha kuwafanya waamuzi wetu wawe bora zaidi, lakini pia tutaunda
kamati ya kuwachunguza waamuzi wote kila mara ili kubaini maendeleo yao,
hii itakuja mara baada ya kuwaongezea ujuzi,” alisema Kidao ambaye ni
mchezaji wa zamani wa Vijana ya Ilala.
Kwa
upande wa uwepo wa madai ya waamuzi hao, Kidao alisema: “Kweli
tunadaiwa, lakini tunadaiwa michezo ya raundi saba kati ya zile 19 hadi
20 ambazo timu zimecheza, lakini suluhisho la hili, tupo katika mikakati
ya kupata wadhamini ambao watakuwa wanashughulikia malipo yao tu.
“Kwa
msimu mmoja, waamuzi wa Ligi Kuu Bara, wanalipwa zaidi ya Sh bilioni
moja, ambapo wadhamini wetu wanatoa Sh milioni 426 kama fedha za malipo
kwa waamuzi, fedha inayobaki ambayo ni zaidi ya Sh milioni 600,
zinalipwa na TFF, Kwa hiyo tunataka kuepusha hili kwa kutafuta wadhamini
wao

0 comments:
Post a Comment