Sunday, August 30, 2020


Wachezaji wa Arsenal wakishangilia na Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Liverpool jioni ya leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
Arsenal ilitangulia kwa bao la Nahodha wake, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 12 kabla Takumi Minamino kuisawazishia Liverpool dakika ya 73. Waliofunga penalti za Arsenal ni Reiss Nelson, Ainsley Maitland-Niles, Cedric Soares, David Luiz na Aubameyang na za Liverpool walifunga Mohamed Salah, Fabinho,  Minamino na Curtis Jones,wakati Rhian Brewster alikosa

 

0 comments:

Post a Comment