Sunday, August 23, 2020

Fainali ya Champions League: Kwanini mechi Bayern vs PSG inasubiriwa kwa hamu?

PSG striker Neymar and Bayern Munich striker Robert Lewandowski

Kunatarajiwa mashambulizi makali katika fainali ya Champions League Jumapili hii, anasema mchambuzi wa soka Barani Ulaya Micah Richards.

Timu zote mbili zinapenda kucheza mpira na huenda zitakuwa zinasema 'wacha tuone ni nani atakayefunga mabao mengi zaidi', katika mechi hiyo itakayochezwa mjini Lisbon.

Bayern Munich ni sawa na mashine na itakuwa vigumu sana kuwadhibiti, lakini Paris St-Germain ina wachezaji wenye talanta ambao hawawezi kuwapuuzwa.

''Kusema kweli siwezi, kubashiri mshindi - Lakini nina hakika kutafungwa mabao. Kibarua sasa ni timu gani itakayotumia vizuri nafasi yake muhimu,'' anasema Richards.

Pengine unaweza kusema hivyo kuhusu mechi kadhaa tofauti lakini katika uchambuzi huu BBC Michezo inaangazia sababu zifuatazo;

Kasi ya 'PSG' inaweza kuiadhibu Bayern'

Graphic showing the Bayern team that beat Chelsea, Barcelona and Lyon: Neuer, Kimmich, Boateng, Alaba, Davies, Goretzka, Thiago, Gnabry, Muller, Perisic, Lewandowski
Maelezo ya picha,

Bayern imechezesha timu moja katika mechi zilizopita za Champions League mji Lisbon, dhidi ya Chelsea, Barcelona na Lyon, na kufunga mabao 15 katika mechi hizo, na kushindwa mara. kwa jumla wamefunga mabao 42 katika mechi 10 za Ulaya msimu huu, hali inayowaweka kifua mbele katika ufungaji wa mabao katika kila mechi kwenye hisstoria ya mashindano hayo

Micah Richards anaongeza: ''Timu ya Bayern inakupatia nafasi nyingi- tuliona hilo katika mechi zao dhidi ya Barcelona na Lyon.''

Hakuna hata moja kati ya timu hizo zilifaulu kutumia nafasi walizopewa wakati mchezo ulipokuwa ulipokuwa imara, lakini tunasubiri kuona jinsi Bayern itakavyacheza PSG wakiwa kifua mbele mara hii.

''Sio kwamba napuuza PSG haiwezi kudhibiti kasi ya Bayern, lakini timu hiyo ya Ujerumani ina kasi kubwa ambayo wachezaji kama Kylian Mbappe na Neymar hawata weza kutumia kupenya lango lao.''

Bayern - wanacheza mechi ya 29- bila kufungwa na tayari wameshinda nyumbani mara mbili - lakini jinsi wanavyotumia mabeki wao kucheza katika safu ya mashambulizi ya wapinzani wao huenda ikawa hatari watakapokutana na timu imara kama PSG.

Graphic showing PSG's team that beat RB Leipzig in the semi-final. If Keylor Navas recovers from the hamstring injury he sustained against Atalanta in the quarter-finals, he could replace Sergio Rico in goal
Maelezo ya picha,

Kikosi cha PSG kilichoinyuka RB Leipzig katika mechi ya nusu fainali. Ikiwa Keylor Navas atapona jeraha alilopata katika mechi dhidi ya Atalanta katika robo fainali, huenda akachukua nafasi ya Sergio Rico

''Nilipenda sana kutazama mkondo wa mwisho ya mashindano ya mwaka huu siku chache zilizopita na mechi hii ya bila shaka itakuwa ya kusisimua, kwasababu kuna mambo mengi ya kukumbuka''. anasema Richards.

Katika mkondo huo wa mwisho wa mashindano timu zilikuwa na kila sababu ya kuwa na hofu kwasababu zilijua lazima zishinde ama zikose nafasi ya pili.

Hali hiyo hiyo inatarajiwa katika fainali. Ikiwa itafikia matarajio ya wengi, basi kivumbi kitashuhudiwa.

'Muller inaogofya'

Changamoto inayokabili timu yoyote inayokutana na Bayern ni jinsi ya kuwadhibiti.

Wakidhibitiwa katika safu ya kati, wanageuza mkondo wa mashambulizi. Ndio, Robert Lewandowski ashawahi kufunga mabao kadhaa ya namna hiyo msimu huu, lakini pia wanatumia mbinu zingine hatari.

Bayern's Poland striker Robert Lewandowski has scored 55 goals in all competitions this season, including 15 in the Champions League. He has scored in each of the nine European games he has played in 2019-20
Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Bayern na Poland Robert Lewandowski amefunga mabao 15 katika Champions League msimu huu.

Mchezo wa Serge Gnabry - ni wa kuridhisha licha ya kwamba hakuwa akiaminika miaka kadhaa iliyopita. Ivan Perisic ni hatari pia alafu kuna Thomas Muller.

''Naweza kusema kwama kutokana na tajiriba yake Muller anawatia kiwewe wachezaji wengi. Cha ajabu hata ukimwangalia hana kasi vile ama nguvu na wala hana ujuzi wa kiufundi vile, lakini ni mchezaji hodari''. Micah Richards alimwambia mwandishi wa micezo wa BBC Chris Bevan.

Anasema kuwa mchezaji huyo amejinasibisha kutokana na uwezo wake wa kujitafutia nafasi au kuwatafutia wenzake nafasi upande wowote wapinzani wao.

''Huwezi kupepesa macho hata sekunde moja ukiwa naye uwanjani kwani atakuadhibu. Amekuwa kibarua kigumbu kwa walinzi kutokana na jinsi anavyopangia mashambulizi - ukimshutukia kumekucha.''

Graphic showing where Bayern Munich's Thomas Muller touched the ball against Barcelona (l) and Lyon (r)
Maelezo ya picha,

Mchoro unaoonesha wakati mchezaji wa Bayern Munich,Thomas Muller alipogusa mpira dhidi ya Barcelona (kushoto) na Lyon (Kulia)

Richards anafananisha umahiri wa Muller na mchezaji mwezake wa zamani wa Manchester City James Milner kwasababu hakubali kushindwa.

''Huwezi kuchukua mpira kutoka kwake kwa njia rahisi kwasababu anausoma mchezo vizuri.''

Yeyote kata ya wachezaji wanne wa safu ya mashambulizi ya Bayern anaweza kuamua matokeo ya mechi, bila kusahau mabeki wao pia. Alphonso Davies alimfanya Nelson Semedo wa Barcelona kuonekana kama mwanagezi wa soka katika mechi ya robo fainali.

Makabiliano yake na Angel di Maria na upande wa kushoto wa Bayern utakuwa wakufuatiliwa, sawa na Mbappe dhidi ya Joshua Kimmich upande wa kulia.

PSG huenda ikawatumia Mbappe na Di Maria kupenya lango la Bayern, lakini pia watalazimika kusaidia safu ya kati jambo ambalo timu zote zitafanya kutuliza mpira katika maeneo hatari.

Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe
Maelezo ya picha,

Mbappe ni mchezaji soka mwenye kasi zaidi duniani, kwa mujibu wa data kutoka kwa gazeti la Ufaransa la Le Figaro, alifikia kasi ya kilomita 36 kwa lisaa limoja

'Boateng hawezani na kasi ya Mbappe - na hakuna mwingine anayewezana nae'

Mchambuzi wa soka Micah Richards, anasema haoni Bayern wakibadili mfumo wao wa mchezo siku ya Jumapili, japi wanajua PSG wana wachezajiambao wanaweza kuwaadhibu wakizembea katika safu ya ulinzi.

''Jerome Boateng ni mmoja wa walinzi hodari duniani, lakini unaweza kumpita ukiwa makini. Nilicheza naye City na wakati mwingine yeye pia hukosea hesabu zake.''

Anasema Davies husaidia sana katika safu ya kati lakini Boateng akiachwa peke yake katika eneo hilo, hatawezana na kasi ya Mbappe - na hakuna mchezaji mwingine anayewezana naye katika hilo.

Naamini Mbappe anaweza kutumia nafasi yoyote ya ufungaji bao. Mchezo wake unakaribia kiwango cha Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwa sasa na sijawahi kuona mchezaji mzuri kiufundi aliye na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi -ikibidi afanye hivyo. Uwezo huo ni nadra sana kwa mchezaji aliye na miaka 21.

Alafu kuna Neymar, ambaye wakati mwingine anaudhika kumtazama akipoteza nafasi kama alivyofanya katika mechi yao dhidi ya Atalanta awamu ya robo fainali, lakini pia anaweza kubadili mkondo wa mchezo kimiujiza.

Neymar akishanglia ushindi wa Champions League akiwa Barcelona 2015
Maelezo ya picha,

Neymar akishanglia ushindi wa Champions League akiwa Barcelona 2015. Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil alijiunga na PSG mwaka 2017

Alipoondoka Barcelona na kuhamia PSG mwaka 2017 baadhi ya watu waliona kama alifanya makosa, lakini akishinda kombe la Champions League trophy katika uga wa Estadio da Luz bila shaka atathibitisha uamuzi huo.

Itakuwa fahari kubwa kwake binafsi, na kwa PSG pia. Bila shaka wanahisi huu ni mwaka wao baada ya kufuzu kwa finali ya kwamara ya kwanza - Lakini, baada ya kukabiliano makali msimu huu, sawa na watakavyojivunia Bayern.

 

0 comments:

Post a Comment