
Chanzo cha picha, Getty Images/Reuters/Rex
Tunapozungumzia kuhusu asilimia , basi bila shaka Manchester City iko mbele kama mfuko wa shati kuwa klabu ambayo Lionel Messi atajiunga nayo.
PSG imewasiliana na babake Messi , ajenti wake kwa mara nyengine kuhusu uwezekano wa kumsajili nahodha huyo wa Barcelona , ambaye aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka siku ya Jumanne.
Na pengine cha kushangaza zaidi ni kwamba Juventus imeanza kuandaa mipango ya kifedha ambayo inaweza kuwafanya Messi na Ronaldo kucheza katika timu moja kwa mara ya kwanza.
Itakuwa timu kali zaidi. Lakini uwezekano huo pia huenda haupo .
Mwisho wa wiki iliojaa vichwa tofauti vyenye uvumi wa uhamisho wa Messi , kuna vitu viwili tunavyojua kufikia sasa .
Messi anataka kuondoka Barcelona na kwamba Barcelona ingependelea sana mshambuliaji huyo wa Argentina kusalia.
Suala hilo ni rahisi, lakini pia linaonekana kuwa gumu zaidi kwasababu pande zote zimeshawishika kwamba sheria ya tarehe 10 mwezi Juni - ambayo inamwezesha Messi kuondoka kama mchezaji huru - pia inawapatia haki kutetea msimamo wao.
Messi anafikiria kwamba anaweza kuondoka bila kulipa chochote kwasababu tarehe hiyo ilitarajiwa kuwa mwisho wa msimu.
Hatahivyo , mlipuko wa virusi vya corona ulimanisha kwamba kampeni hiyo ilikamilika kwa mchuano wa fainali ya kombe la ligi ya mabingwa tarehe 23 Agosti , siku mbili kabla ya Messi kuiambia Barcelona kwamba anataka kuondoka rasmi.
Barca inaamini kwamba muda wa yeye kuonesha lengo la kuondoka uliisha na kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 atakamilisha kandarasi yake miwsho wa msimu wa 2020-21.
Mawakili watakuwa wakiramba vidole vyao wakisubiri.

Chanzo cha picha, Getty Images
LIonel Messi amejishindia mataji sita ya Ballon d'Or kama mchezaji wa Barcelona
Lionel Messi has won six Ballons d'Or as a Barcelona player
Kulingana na Messi hakuna kilichobadilika . Angependelea kuondoka na msharti mazuri zaidi.
Barcelona imesema kwamba haimuuzi mchezaji huyo - isipokuwa iwapo mtu mwengine anafikiria kuondoa kifungo cha Yuro Milioni 700 zitakazohitajika katika uuzaji wake wakati huu .
Messi hataki kuondoka kwa njia mbaya , sio kwasababu ya bodi lakini kwasababu ya heshima alionayo kutoka kwa klabu hiyo na mashabiki. Wengi wanaangazia barua aliotuma kwa Barcelona kuhusu lengo lake la kutaka kuondoka , wakisema kwamba ilikuwa njia ya ukosefu wa heshima.
Sio hivyo. Messi alikuwa amewaambia kwa mdomo mara kadhaa kuhusu lengo lake la kutaka kuondoka .
Mpango wa Messi haujabadilika wakati wote huo. Mabadiliko yatakuwa iwapo anataka kuzua mtafaruku kati yake na klabu hiyo.
Raia huyo wa Argentina hana mipango ya kutoa taarifa katika siku za hivi karibuni, huku ikiwa kuna mengi ya kujadiliwa .
Wakati mambo yatakapoanza kuchukua mkondo mzuri, Messi atakuwa yuko tayari kuzungumzia hisia zake lakini sio kabla.
Wachezaji ni sharti wafanyiwe vipimo kabla ya kuanza kwa msimu mpya siku ya Jumapili na baadaye mazoezi yaanze siku ya Jumatatu.
Uvumi kwamba Manchester City itawaachilia wachezaji wake muhimu kuondoka ili kutoa fursa kwa Messi sio wa kweli.
Mabeki Angelino au Eric Garcia wanaweza kujumuishwa katika makubaliano.
Hakuna klabu ambayo inaweza kulipa dau la uhamisho la Yuro Milioni 100 pamoja na mshahara wa Messi ikitazamiwa kwamba mshahara wake utapunguzwa kokote aendako.
Barcelona haitakubali ubadilishanaji wa wachezaji , hawamtaki mchezaji yeyote kutoka City.
Hawataki kuuza na watajiandaa kukutana na Messi kuongeza mkataba wake , lakini sio kujadiliano kuhusu uhamisho wake.
Josep Maria Bartomeu sio rais wa klabu ya Barcelona ambaye anataka Messi kuondoka.
Lakini je anafikiria nini? Kwa kweli sio klabu, kwasababu anapanga kumzuia mchezaji asiyefurahia kusalia na ambaye anaweza kuondka baada ya miezi 12.
Kuondoka kwa Messi kutaruhusu wachezaji wengine kukua na kuimarika msimu ujao. Na hawa ni wachezaji gani. Frenkie de Jong, Miralem Pjanic, Antoine Griezmann, Ousmane Dembele, Philippe Coutinho, Gerard Pique na Marc-Andre Ter Stegen kwa ufupi.
Watalazimika kununua kiungo wa kati na beki wa kati hivi sasa.
Kwa kusisitiza kwamba haitamruhusu Messi kuondoka kutakuwa kutoona mbali kwa Bartomeu.
Tunasubiri kuona ni hatua gani inachukuliwa baadaye, tukianza na iwapo Messi atahudhuria mazoezi siku ya Jumatatu au la.
0 comments:
Post a Comment