
Nyota wa Barcelona Lionel Messi
Baba yake Lionel Messi amewasili nchini Uingereza kuzungumzia kandarasi ya miaka miwili na klabu ya Manchester City baada ya mshambuliaji huyo wa Argentina ,33, kusema kwamba anataka kuondoka Barcelona.. (Sun)
Iwapo makubaliano hayo yataafikiwa yataigharimu City £500m. (Telegraph)
Klabu yoyote inayotaka kumsajili Messi italazimika kulipa £90m kwa mwaka ili kufikia mshahara wake anaolipwa. (Times - subscription required)
Messi atashiriki katika mazoezi siku ya Jumatatu ili kuepuka matatizo yoyote ya kisheria na klabu hiyo.. (Sport - in Spanish)
Manchester United ina fedha za kumnunua Messi lakini winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, ndio lengo lao kuu . (Express)
Mshambuliaji wa Barcelona na Uruguay Luis Suarez, 33, aliitwa na mkufunzi mpya Ronald Koeman siku ya Jumatatu na kuambiwa anahitaji kutafuta klabu nyengine. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez
Winga wa Bournemouth na Wales David Brooks ameorodheshwa miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza kuhama na kwamba tayari klabu ya Manchester United inamnyatia iwapo haitaki kulipa £108m kumnunua Sancho. (Express)
Ombi la klabu ya Manchester United la kutaka kumnunua kwa dau la £22m beki wa Ufaransa Benoit Badiashile, 19, limekataliwa na Monaco. (RMC via Star)
Tottenham inakaribia kumnunua beki wa kulia wa klabu ya Wolverhampton Wanderers Matt Doherty. Wolves wanataka kulipwa £20m ili kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Jamhuri ya Ireland lakini Spurs inataka kulipa kitita cha chini ya dau hilo. (Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images
Benoit Badiashile
Mchezaji nyota wa Bayern Munich Thiago Alcantara yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo iliotawazwa mabingwa wa Ulaya . Klabu hiyo ya Bundesliga inataka dau la £30m huku Liverpool ikihusishwa na kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 29. (Express)
Brighton imejiandaa kumzuia beki wa England mwenye umri wa miaka 22 Ben White , ambaye alihudumu kipindi chote cha msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Leeds, licha ya hamu kutoka kwa Liverpool, Chelsea na Manchester United. (Sun)
Mchezaji huru Edinson Cavani amekataa uhamisho wa kueleka Juventus kutokana na utiifu wake na klabu yake ya Napoli. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliondoka Paris St-Germain mwisho wa msimu uliopita. (Sky Sports Italy, via the Mail)

0 comments:
Post a Comment