Saturday, August 22, 2020


Gabriel Magalhaes
Maelezo ya picha,

Arsenal wanakaribia kumsajili beki wa Lille Gabriel Magalhaes

Arsenal wanakaribia kukamilisha mchakato wa uhamisho wa Gabriel Magalhaes. Gunners wametoa ofa ya mkataba wa miaka mitano, kumpata beki huyo aliye na umri wa mika 22- raia wa Brazil lakini Napoli hawajakatiza matumaini ya kumsajili. (Times - subscription required)

Napoli wakimkosa Gabriel, huenda wakamnunua beki Arsenal Mjerumani Shkodran Mustafi. (Daily Star)

Manchester United pia wako mbioni kumsaka Gabriel, lakini lazima waongeze ofa yao kumpata. (Daily Star)

Manchester United wametoa ofa ya £27m kumnunua winga wa Juventus na Brazil Douglas Costa, 29, lakini klabu hiyo ya Serie A inataka kulipwa £9m zaidi. (Joe)

Chelsea wanakaribia kumpata winga wa Ujerumani Kai Havertz ,21, baada ya kufanya mazungumzo zaidi na Bayer Leverkusen kuhusu bei yake. (Guardian)

Douglas Costa
Maelezo ya picha,

Manchester United wametoa ofa ya £27m kumnunua winga wa Juventus na Brazil Douglas Costa

West Ham wanajaribu kumuuza kiungo wa kati wa England Jack Wilshere, 28, na wako tayari kulipa mwaka mmoja uliosalia katika mkataba wake ama kupunguza ada ya kumwezesha kuhamia klabu nyingine. (Times - subscription required)

Chelsea wameongeza juhudi za kumsaka nahodha wa Paris St-Germain Thiago Silva, huku beki huyo wa mwenye umri wa miaka 35- wa Brazil akiwa tayari kucheza Jumapili katika finali ya Champions League dhidi ya Bayern Munich siku ya Jumapili. (The Athletic - subscription required)

Thiago Silva
Maelezo ya picha,

Chelsea wameongeza juhudi za kumsaka nahodha wa Paris St-Germain Thiago Silva

Kipa wa Lille Mike Maignan, 25, ananyatiwa na Chelsea. (Le10 Sport via Star)

Manchester City wameafikiana na Napoli kuhusu usajili wa beki wa Senegal Kalidou Koulibaly, 29. (Sports Illustrated)

Wachezaji wenza wa Jadon Sancho katika kblabu ya Borussia Dortmund wana imani nyota huyo wa England mwenye umri wa miaka 20 - ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuenda Manchester United - atasalia katika klabu hiyo ya Bundesliga kwa mwaka mwingine mmoja baada ya kushiriki mazoezi ya kabla ya kuanza kwa msimu. (Telegraph - subscription required)

Jordan Sancho
Maelezo ya picha,

Jadon Sancho, winga wa Borussia Dortmund

Paris St-Germain inamnyatia beki wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, 21. (O Jogo - in Portuguese)

Liverpool inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara huku mchezaji huyo wa Uhispania, 29, akipatikana kwa pauni milioni 30. (Independent)

Kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman anataka kumleta kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 29, Nou Camp. (Algemeen Dagblad, via Express)

 

0 comments:

Post a Comment