Monday, August 24, 2020

mshambuliaji wa Celtic Mfaransa Odsonne Edouard

Newcastle wametoa ofa ya £4.5m kwa klabu ya Ugiriki ya PAOK kumnunua mchezaji wa safu ya kushoto - kulia Mgiriki Dimitris Giannoulis,24. (Manu Lonjon via Sports Lens)Mkufunzi mpya wa Barcelona Ronald Koeman

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anapania kumvuta kocha wa Brentford na mtaalamu Andreas Georgson kuwa sehemu ya kikosi cha ufundi. (London Standard)

Mshambuliaji wa klabu ya Tromso raia wa Norway Isak Hansen-Aaroen, 16, amethibitisha katika mitandao ya kijamii kuwa atahamia Manchester United. (Mirror)

Mike Arteta

Luis Figo hatarajii mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, akifuata nyayo zake kwa kuondoka Barcelona na kuhamia Real Madrid. (Marca)

Mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 38, bado hajasaini mkataba mpya AC Milan. Mchezaji nguli huyo atasalia bila timu mkataba wake utakapo kamilika mwisho wa mwezi Agost. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mshambuliahi wa Juventus Cristiano Ronaldo "alimpendekeza" kiungo wa kati raia wa Portugal Bruno Fernandes, 25, kwa Manchester United, kulingana na beki wa zamani wa United Patrice Evra. (The Guardian)

 

0 comments:

Post a Comment