SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hana tatizo na nyota namba moja wa kucheza na nyavu ndani ya Simba Meddie Kagere.
Habari
zinaeleza kuwa wawili hao walipigana jana baada ya kutofautiana jambo
ambalo lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku uongozi wa Simba
ukikanusha kwamba hakuna ukweli katika hilo.
Sven amesema kuwa:- "Siwezi
kutumia nguvu kwenye mambo yasiyo ya maana ambayo sijui yanatoka wapi.
Mimi sina tatizo, Medie hana tatizo hilo ndilo ninaweza kusema."
Kagere
ndani ya Bongo kwa misimu miwili mfululizo amesepa na tuzo ya mfungaji
bora ambapo msimu wa 2018/19 ikiwa ni msimu wake wa kwanza alitupia
mabao 23.
Msimu wa 2019/20 alitupia mabao 22 na kufanya afikishe jumla ya mabao 45 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Kwa
sasa Simba imeanza maandalizi ya mchezo wao wa ligi unaotarajiwa
kuchezwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine, Mbeya dhidi ya Ihefu.
0 comments:
Post a Comment