Saa 3 zilizopita
Wakati Joan Laporta alipochaguliwa kuwa rais wa Barcelona mwezi March, moja ya vitu ambavyo aliviweka wazi mapema kabisa ni kuhusu kocha Ronald Koeman kwamba hayuko kwenye mipango yake ya muda mrefu.
Miezi sita baadae, Six months later, anakuja na mapendekezo mengine akikaribia kumuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja mholanzi huyoi.
Lakini miezi sita na wiki mbili baadae , kinachoonekana kitu pekee kinachomfanya Koeman aendelee na kazi hiyo ni ukweli kwamba akiondoka atatakiwa kulipwa fedha nyingi. Na hilo ndio bodi ya timu hiyo inalitizama wakati huu- kukiwa na mtikisikio wa kifedha.
Kwanini Laporta amekuwa kigeugeu wa fikra?
Haishangazi, sula la pesa ndo msingi wa yote, kwa upande wa Barcelona, wana tatizo la kifedha. Bila kumungunya maneno, kwa sasa hali ya kifedha Barcelona ndiyo inaamua masuala yote.
Lakini hali inazidi kuwa ya wasiwasi kati ya Rais na Meneja ambae klabu inafikiria kusaka mbadala wake, ikitegemewa na matokeo ya mechi chache zijazo, inawezekana wakatumia kiwango kidogo cha pesa ilicchonacho kuachana na Meneja huyo ambaye inaonekana haendi sawa na klabu kwa sababu anafikiri amesdalitiwa.
Roberto Martinez, ambaye anataka kuendelea kuionoa timu ya taifa ya Ubelgiji angalau mpaka mashindano ya Ulaya ya Nations League yaishe, ni mmoja wa makocha wanaotajwa kuwaniwa kuziba nafasi yake.
Kwa namna gani imefikia hapa?
Laporta na Koeman walikutana kabla ya kuanza kwa msimu mpoya. Wakiwa wnaakula chakula cha mchana, Laporta alimtaka mholanzi huyo kumpa siku 14 kuamua kama klabu itaendelea kuwa nae ama la, lakini kuliweka vizuri hili katika namna nyingine, siku 14 hizi ni kuona kama wanaweza kumpata mbadala wanayemuona anafaa kwa kazi hiyo.
Wakala wa Koeman, Rob Jansen, ameiweka vizuri hili: "Fikiria: Nataka kukuoa, sina shaka a hilo. Nipe wiki mbili nitafute mwenza sahihi. Kama sitampata mtu sahihi, tutaoana"
Hakumpata mwenza huyo. Wakati huo Laporta hakutaka kumrejesha kiungo wa zamani na gwiji wa Barca, Xavi na haikuwezeka kabisa kumpata Julian Nagelsmann, ambaye anapendwa sana na Laporta kwa sababu ya soka lake la kisasa. Kocha huyo hakutaka kuikacha Bayern Munich na kutimkia Barcelona, akiwa tayari ameshafikia makubaliano na Bavarians hao.
Hali hiii haijaanza sasa, imerithiwa kutoka uongozi uliopita na kusababisha klabu hiyo kuwa katika hali ngumu iliyonayo sasa. Koeman angeweza kupatiwa mkataba wa mwaka mmoja. Rais aliyepita Josep Maria Bartomeu - yeye alimpatia miaka miwili kwa kuanzia.
Hali imefikia pabaya sasa, Barcelona ikimtimua itapaswa kumlipa kitita kinono. Wiki iliyopita, TV3 iliripoti kiwango kikubwa cha euro milioni 12m anazoweza kuweka kibindoni.
Kwa manenpo mengine, Koeman analipwa vizuri, aendelee na kazi ama afukuzwe ama aongezewe mkataba. Hilo ni alama nyingine mbaya iliyoachwa na utawala wa Bartomeu.
Rais wa Barcelona Joan Laporta aliweka wazi mwezi Agosti mwaka huu kuwa klabu hiyo ina madeni ya £1.15bn
Tangu amewasili Koeman amefanya kila aliloagizwa afanye na klabu hiyo, ikiwemo kuwaondoa magwiji wa klabu hiyo akiwemo Luis Suarez aliyerushiwa virago kwa njia ya simu ambayo haikuchukua hata sekunde 90.
Na alikuwa Koeman aliyeambiwa ashughulikie suala la kutimka kwa Lionel Messi na Antoine Griezmann walioondoka siku ya mwisho ya usajili. Alikuwa mholanzi huyo aliyefuata mapendekezo ya klabu ya kuwatumia na kuwekeza zaidi kwa vijana aliowaingiza kwenye mifumo yake.
Mechi iliypota ya ligi ya mabingwa Ulaya waliyofungw ana Bayern, alikuwa na vijana kama Yusuf Demir (18), Alex Balde na Gavi (wote wana miaka 17) walioungana na kinda wa miaka 18 Pedri, baada ya kipyenga cha mwisho kikosi cha Barcelona kilionekana kama cha shule ya chekechea.
Koeman, ambaye ana wachezaji 8 tegemeo majeruhi akiwemo Ousmane Dembele, Sergio Aguero na Ansu Fati (mwenye miaka 18), anasisitiza kwamba ataendelea kutumia vijana. Mashasbiki wanaonekana kukubaliana na hilo, licha ya kuonekana makinda hao hawako tayari kwa viwango vyao kubeba mzigo huo. Mashabiki wanaamini muda mfupi ujao wataona sura walizozizoea.
Kwa sasa Koeman ataendelea kufanya anachoona kinafaa.
Baada ya kipigo kutoka kwa Bayern, Laporta alikutana na wakurugenzi kadhaa kuangalia nini cha kufanya. Kwa mara ya kwanza katika historia ya ligi ya mabingwa Ulaya, Barcelona haijafanikiwa kupiga shuti hata moja langoni mwa wapinzani wao.
Koeman hakutaka kuficha ukweli kwamba alicheza mchezo huo ili kujiinda asifungwe mengi na wala sio kutafuta ushindi. "Tungecheza kwa kujiachia, tungefungwa zaidi," alisema. Kama Laporta angelikuwa na pesa na angepatikana mtu sahihi aliye tayari, kumrithi Koeman, mholanzi huyo akitimuliwa.
Mvutano huu wa kimuelekeo kati ya Laporta na wanachokitaka Barcelona na ukweli wa hali halisi ya mambo ulivyo, na ndio upande alipo Koeman, ni vigumu kuona namna gani wanaweza wakaachana kwa Amani na furaha.
0 comments:
Post a Comment