Wednesday, September 22, 2021

 

Lewandoowski mfungaji bora Barani Ulaya

   Muungwana Blog 2        Sep 22, 2021



Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowski (33) amekabidhiwa tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu tano bora barani Ulaya 'European Golden Shoe' baada ya kufunga mabao 41 kwenye michezo 28 ya Bundesliga msimu uliopita wa mwaka 2020-21.

Lewandowski amekabidhiwa tuzo hiyo leo Septemba 21, 2021 baada ya kuwapiku wafungaji bora wa Ligi nyingine, Harry Kane wa Tottenham Hotspurs aliyefunga mabao 23, Cristiano Ronaldo aliyekuwa Juventsu aliyefunga mabao 29 na kuwa mfungaji bora wa Serie A.

Kwa upande wa La Liga amempiku mfungaji bora wa Ligi hiyo Lionel Messi aliyekuwa Barcelona na kufunga mabao 30, na Kylian Mbappe wa PSG aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi kuu ya Ufaransa maarufu 'Ligue 1'.

Mara baada ya kuchukua tuzo hiyo, Lewandowski amesema anawashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano mkubwa waliompatia mpaka kumfanya awe mfungaji bora na kuwa na msimu bora wa mafanikio kwa kutwaa mataji yote waliyokuwa wanashindania kwa msimu wa mwaka 2019-2020.

Robert Lewandowski amechukua tuzo hiyo kwa mara yake ya kwanza na kumpora mshambuliaji wa Lazio na timu ya tiafa ya Ital, Ciro Immobile aliyechukua tuzo hiyo msimu juzi wa mwaka 2019-2020 kwa kufunga mabao 36.

0 comments:

Post a Comment