Monday, September 27, 2021

 Imepakiwa mnamo 2:42

Mshambuliaji wa kenya Michael Olunga
Image caption: Mshambuliaji wa kenya Michael Olunga

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Michael Olunga, amefungia klabu yake ya Al Duhail mabao matano katika mechi ya kusisimua ya ligi ya mabingwa nchini Qatar siku ya Jumapili,

Ushindi huo dhidi ya Al-Sailiya imeiwezesha Al Duhail kuongoza msimamo wa ligi.

Olunga aliyengia uwanjani kama mchezaji wa ziada katika kipindi cha pili aliwezesha timu yake kuongoza msimamo wa jedwali la ligi hiyo.

Alikuwa amekosa mechi mbili baada ya kujeruhiwa lakini alirerejea kwa kishindo na kuiwezesha timu yake kunyakua alama zote tatu muhumu.

Mshambuliaji huyo wa Kenya aliingia kwenye mechi hiyo katika dakika ya 46 na kuchukua chini ya dakika 10 kufungu bao.

Social embed from twitter

0 comments:

Post a Comment