![IMG-20170525-WA0016[1]](https://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/05/IMG-20170525-WA00161.jpg)
Matajiri wa Mkoa wa
Singida ambao wamepanda Ligi Kuu Msimu huu wameanza kujiweka fiti katika
usajili wa wachezaji wa ndani na mchezaji wa kwanza kusaini ni Kiungo
Mkabaji wa Mbeya City, Kenny Ally MWambungu sasa ni mali ya Singida
United.
Huu ni usajiri wa
sita baada ya kuwasajili wachezaji watano wa kigeni na kwa mujibu wa
katibu Mkuu wa klabu hiyo inataka kusajili jumla ya wachezaji 14.
Kenny Ally alikuwa
kwenye vichwa vya habari katika timu kubwa zilizokuwa zinawaania saini
ya mchezaji huyu wakiwemo wakongwe Simba na Yanga na nyingine kama vile
Azam FC,Mwadui Fc.
Singida United ambayo
ipo chini ya Kocha mwenye mafanikio Tanzania hata bara la Afrika na
mwenye uzoefu wa Ligi Hans Van Der Pluijm ambaye alikuwa kocha wa Zamani
wa Mabingwa wa Kihistoria Yanga ambapo aliwapa mataji mawili mfululizo
hata huu ubingwa wa tatu unachangizwa na Juhudi zake kwani aliiongoza
Msimu wa kwanza na msimu wa pili alimuachia George Lwandamina
0 comments:
Post a Comment