Mechi hizo, zinazoitwa Ziara 2017, zitaanzia huko Marekani ambako watacheza Mechi 5 dhidi ya LA Galaxy, Real Salt Lake, Real Madrid, Barcelona na Manchester City, nah ii ndio itakuwa Dabi ya kwanza kabisa kuchezwa nje ya Uingereza.
Baada ya Ziara hiyo ya huko USA, Man United wataruka kwenda huko Oslo, Nchini Norway kucheza na Klabu ya huko Valerenga na kisha kwenda Dublin Nchini Ireland kucheza na Sampdoria ya Italy.
Mechi hizo zitaanza Julai 15 na kumalizika Agosti 2.
Msimu Mpya wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, utaanza Agosti 12 na kumalizika 13 Mei 2013 wakati Ratiba ya Msimu huo itatangazwa Juni 14.
Akiongelea kuhusu Ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, ameeleza kuwa Mechi hizo zitawapa changamoto tofauti na pia kuwapa nafasi Mashabiki wao maeneo mengi tofauti kuona Timu yao huku pia zikimpa Meneja nafasi ya kutathmini Timu dhidi ya Timu pinzani nzuri na zenye nguvu.
MAN UNITED - RATIBA KAMILI:
Jumamosi 15 Julai - LA Galaxy; StubHub Center, Carson, California, USA
Jumatatu 17 Julai - Real Salt Lake; Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah, USA
Alhamisi 20 Julai - Manchester City; NRG Stadium, Houston, Texas, USA
Jumapili 23 Julai - Real Madrid; Levi’s Stadium, Santa Clara, California, USA
Jumatano 26 Julai - Barcelona; FedEx Field, Landover, Maryland, USA
Jumapili 30 Julai - Valerenga; Ullevaal Stadium, Oslo, Norway
Jumatano 2 Agosti - Sampdoria; Aviva Stadium, Dublin, Ireland
0 comments:
Post a Comment