- Details
- Created: Wednesday, 21 June 2017 06:24
Tayari Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Egypt mwenye Miaka 25 ameshaafiki Maslahi binafsi na Liverpool.
Mapema Mwezi huu, AS Roma waliigomea Ofa ya Liverpool ya Pauni Milioni 28.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amevutiwa mno na Salah ambae Msimu uliopita aliifungia AS Roma Bao 19 na kusaidia 15 katika Mechi 41 na kuiwezesha AS Roma ikamate Nafasi ya Pili kwenye Serie A nyuma ya Mabingwa Juventus.
Salah aliwahi kuwa Mchezaji wa Chelsea kati ya 2014 na 2015 na kucheza Mechi 19 tu kisha kupelekwa kwa Mkopo huko Italy kwa Klabu za Fiorentina na AS Roma na Agosti 2016 kuhama moja kwa moja kujiunga na AS Roma.
Ikiwa Dili hii itagonga hiyo Pauni Milioni 39 basi itavunja Rekodi ya Liverpool kumnunua Mchezaji kwa Bei ghali tangu walipomnunua Andy Carroll Mwaka 2011 kwa Pauni Milioni 35.
Pia, itaweka Rekodi kwa kuivunja ile Liverpool waliyomnunua Sadio Mane kwa Pauni Milioni 34 na kumfanya awe Mchezaji wa Bei ghali kutoka Afrika.
0 comments:
Post a Comment